Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 21, 2013

BONDIA KALAMA NYILAWILA AWAASA MABONDIA KUACHA USHILIKINA

BONDIA Kalama Nyilawila 
BONDIA  Karama Nyilawila amewataka mabondia wa Tanzania kuacha imani
za kishirikina na badala yake wafanye mazoezi  ili waweze kufikia mafanikio.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nyilawila alisema  hapendezwi na
vitendo hivyo kwani vinauwa viwango vya michezo nchini.
Alisema mabondia wanatakiwa wasiamini kabisa na kwamba wamekuwa
wakifanya mambo hayo wanapoenda kupambana nje ya nchi.
Nawasihi waachane na imani za kishirikina kwani wanapokwenda huko
huishia kupigwa kwa KO ila naamini wakizingatia mazoezi yatawasaidia
kufanya vema,"alisema.
Alisema mazoezi pekee ndiyo yatakayomsaidia bondia kushinda pambano
lake na si kwenda kwa mganga na kumpa nguvu za giza na badala yake
jitihada zake binafsi  ulingoni ndizo zitakazomfaa.
Alisema watu wasitafute mchawi  aliyesababisha Tanzania isifanye vema
kimataifa kwani wachawi ni wanamichezo wenyewe na wengi wamekuwa
wakiamini imani hizo.
Nyilawila alisema kwa sasa yupo katika mazoezi makali chini ya meneja wake
Seleman Zugo na kwamba  amejipanga kushinda mapambano yake yote yaliyopo mbele yake kwa KO raundi za mwanzoni ambambo hivi karibuni bondia huyo alimshinda kwa K,O  ya raundi ya kwanza bondia Kaminja Ramadhani mpambano ulioandaliwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi  Rajabu Mhamila 'Super D' uliofanyika

NOVEMBA 10

 katika ukumbi wa Zulu Paradise pugu kilumba

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...