Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 29, 2013

MABONDIA JAPHET KASEBA, ALIBABA KUZIPIGA DESEMBA 21 FRIENDS CORNER HOTEL DAR


Mabondia Japhet Kaseba wa jijini Dar es Salaam, na Alibaba Ramadhan wa jijini Arusha, wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21 Decemba, mwaka huu katika ukumbi wa friends corner hotel,kuzichapa katika pambano la kirafiki lisilo la ubingwa..
Pambano hilo liloandaliwa na Promota Ibrahim Kamwe chini ya  BigRight Promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia kama Karage Suba na Fadhil Awadh, watakaozichapa kuwania ubingwa wa Mkoa katika uzito wa wealter Kg66 pambano la raundi kumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe, alisema kuwa  zaidi ya hayo mapambano ya ubingwapia mahasimu wawili wa uzito wa juu Lusekelo Daudi atazipiga na  Mbaruku Kheri (ndota) ikiwa ni marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi. 

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni pamoja na Bondia Adam Yahaya (Baby Edo) atazipiga na Harman Richard, mkongwe Enerst Bujiku (Tyson) atacheza na Shah Kassim,  kukumbushia Enzi za akina Stanley Mabesi , Jocky Hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena Rajabu.

Wengine ni Issa Omar  atazipiga na Haji Juma wa Tanga, Moro Best atapigana na Shafii Ramadhan, huku Shaban Bodykitongoji akizipiga na Mwinyi Mzengera. 

Mabondia wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huo na wameshaingia kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.

kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi kutoka Kampuni ya Kiwango Security na jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...