Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 6, 2013

BENKI YA BARCLAYS TANZANIA YAZINDUA RASMI KAMPENI IJULIKANAYO KAMA “ONGEZA AKIBA YAKO” LEO JIJINI DAR Afisa Wa Michezo ya bahati nasibu Abdallah hemed (kushoto) akiangalia moja ya kuponi yenye jina ambalo lilitangazwa mshindi mara baada ya droo ya kutafuta washindi watano wa kampeni ya Ongeza akiba yako inayoendeshwa na benki ya Barclays nchini Tanzania anayeshuhudia Katikati ni Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania Bi Sarah Munema 
Mkuu wa kitengo cha Matawi ya Benki ya Barclays Tanzania Bw Musa Kitoi akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampeni hiyo Mpya iliyozinduliwa leo jijini Dar kwa Droo ya kutafuta washindi watano. Kampeni hiyo ya Ongeza Akiba Yako na Barclays imezinduliwa leo Jijini Dar.
Mmoja wa Washindi Wa Kampeni ya Ongeza akiba Yako inayoendeshwa na benki ya barclays Tanzania (wa pili kushoto) akisoma moja ya kuponi yenye jina la mteja ambaye ameibuka mshindi katika kampeni ya Ongeza Akiba Yako iliyozinduliwa leo kwa kuchezesha droo ya bahati nasibu katika ofisi ya benki hiyo ya Barclays Tawi la Mwenge.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Uzinduzi wa Kampeni ya Ongeza Akiba na Barclays ambayo imezinduliwa leo Katika Tawi la Barcalys Mwenge leo
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
6, Novemba, 2013
Benki ya Barclays Tanzania, Leo hii Imezindua Rasmi Kampeni ijulikanayo kama “Ongeza Akiba Yako” kwa wateja wake. Kampeni hii ilizinduliwa Mnamo Tarehe 16, Septemba, 2013, na inatarajiwa kuendelea Mpaka Tarehe 16, Januari, 2014.
Kampeni hii itawapa fursa wateja watano, (5) kila mwezi, kujishindia mpaka kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni moja kwa kila mmoja katika kipindi chote cha kampeni. Droo ya kampeni itakuwa ikifanyika katika kila wiki ya mwisho wa mwezi, ikiangalia vigezo vya kila mteja.
Akiongea na waandishi wa Habari leo hii, Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wa kawaida, Bwana Musa Kitoi alisema, “Kampeni hii iko wazi kwa wateja wote wa Benki ya Barclays, na wale wapya, kupitia akaunti zao mbali mbali za fedha za Tanzania. Kwa mteja kujipatia nafasi ya kushiriki, mteja anapaswa kutokushuka chini ya kiwango cha shilingi Laki Tatu (300,000). Kiwango hiki kinatakiwa kiwekwe ndani ya mwezi toka kampeni izinduliwe, na kinatakiwa kisishuke kiwango kilichotajwa. Wateja wapya wanaweza kuingia kwenye droo hii pindi tu watakapofungua akaunti zao, na kuweka kiwango kisichopungua shilingi laki tatu. Baada ya kufungua akaunti, na kuweza kubakisha kiwango kilichotajwa kwenye akaunti, wateja, (wa zamani na wapya) wataingizwa kwenye droo ya kila mwezi, na wateja watano (5) watapata bahati ya kuongezewa mara mbili akiba zao, na katika droo kubwa ambayo itakuwa mwisho wa kampeni, mshindi atajinyakulia kiasi kipatacho milioni thelathini, (30,000,000)”.
Aliendelea na kusema, “Leo hii tutapata washindi wetu wa kwanza  watano (5) wa kampeni hii, na Benki ya Barclays inawapongeza wote waliojishindia, na kuwasihi wateja wote kushiriki katika kampeni hii, wakati tukikaribia kipindi cha sherehe za mwisho wa mwaka”.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...