Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 13, 2013

PEMBE ZA TEMBO ZANASWA BANDARINI ZANZIBAR ZIKIWA SAFARINI KWENDA NJE YA NCHI


 
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua magunia yaliokuwa na Pembe za Tembo yaliokamatwa katika bandari hiyoleo yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40. 
Askari wa jeshi la Polisi wakitowa Pembe za Tembo katika makunia wakati wa zoezi hilo leo asubuhi katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Magunia haya yakiwa na sehena na makombe ya pwani wakati katikati yakiwa na viroba vya mPembe za Tembo ambayo yakiwa yamehifadhiwa katika Kontena likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya Zanzibar leo asubuhi. 
Zoezi likiendelea kupekuwa makunia ya Makombe ya Pwani kutowa magunia yaliohifadhiwa Pembe za Tembo 
Baadhi ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar yakisubiri kuhisabiwa kupata idadi kamali na thamani yake na uzito kwa ujumla.
Operesheni ukiendelea kuhesabu Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha hesabu iliokamilika na kupata thamani yake halithi.

Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote.chanzo Hapa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...