Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 7, 2013

MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA TANZANIA WAVUKA MALENGO WA UKUSANYAJI DAMU

Ofisa uhusino na masoko wa Mpango wa Taifa wa damu salama Bw. Rajab Mwenda (kulia) akielezea kuhusu rpoti ya

makusanyo ya damu ya robo mwaka na mikakati ya kukusanya damu kipindi cha Novemba- Januari 2013 wakati wanafunzi

wakiwa likizo


Na Mwandishi Wetu
           
MPANGO wa Taifa wa Damu S
alama Tanzania (NBTS) umevuka malengo ya ukusanyaji  damu   kwa asilimia 110  katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Septemba 2013 ambapo jumla ya chupa 38,552 zilikusanywa na kuvuka malengo ya chupa 35,000 zilizokuwa zikusanywe.
Ofisa Uhusiano na Masoko wa Mpango wa Damu Salama Tanzania Bw. Rajab Mwenda alisema Kanda iliyongoza kwa makusanyo ya damu ni  Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Dodoma na Pwani  ambako jumla ya chupa 13,669 zilikusanywa, Kanda inayofuatia kwa ukusanyaji damu ni Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro,Arusha, Manyara, Tanga)  iliyokusanya chupa 6,159.
Alisema katika kipindi cha mwezi oktoba 2012 hadi Septemba 2013 takwimu zinaonyesha chupa za damu 139,676 ambayo ni sawa na asilimia 99.8 ya lengo la kukusanya chupa 140,000 ilifikiwa hata hivyo Mpango wa Taifa wa damu salama unakusanya asilimia 26 ya mahitaji ya damu kwa mwaka.  Mahitaji ya damu kwa mwaka ni wastani wa chupa 400,000- 450,000.
Alisema tofauti iliyoko ya upatikanaji wa damu kwenye hospitali  nchini imekuwa inafidiwa na ndugu wa wagonjwa  katika kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mgonjwa.
Bw. Mwenda alisema mbalimbali ambazo zinasababisha mpango kushindwa kukusanya damu kwa 100% toka kwa wachangiaji damu wa hiari kunatoakana na uelewa mdogo katika jamii kuhusu uchangiaji damu kwa hiari kwani mfumo uliozoeleka ni ndugu wa mgonjwa ndiyo wanatoa.
Alisema nyingine  ni uhamasishaji usiotosheleza toka kwa viongozi mbalimbali wa jamii, wanasiasa, viongozi wa dini, uuzwaji wa damu usio halali hospitalini jambo ambalo linawakatisha tamaa wachangia damu wa hiari, matumizi yasiyo sahihi ya damu katika hospitali  na miundombinu hafifu hususan barabara duni wakati wa kukusanya na kusambaza damu.
Bw. Mwenda alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama una wadau mbalimbali ambao hujitokeza kuchangia damu kwa hiari kama taasisi za kidini, majeshi, sehemu za kazi, mikusanyiko ya watu na wanafunzi ambao huchangia asilimia 80 ya damu hapa nchini
Alisema katika kipindi cha Novemba hadi  Januari kila mwaka  ni kigumu katika ukusanyaji damu kwani  wadau wakuu ambao ni wanafunzi wanakuwa likizo ya mwaka hivyo Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeweka  mikakati mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Alisema katika mikakati hiyo ni kufanya  kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari  katika jamii na sehemu za makanisani, minadani, stendi za mabasi, misikitini, kwenye masoko na sehemu za kazi.
Alisema wameanza kuhamasisha kambi za jeshi, makundi ya dini na ma wasiliano yamefanyika kwa jumuiya mbalimbali hapa nchini zichangie damu mfano jumuiya ya Khoja shia, Sabato na Jaula.
Pia alisema watatumia vyombo vya habari ili kuikumbusha na kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu  na visaidie kutoa elimu na kutangaza ratiba  ya ukusanyaji damu katika vituo vidogo na vikuu.
Alitoa rai kwa Watanzania kujitokeza kuchangia damu kwa hiari katika vituo vya damu salama kwa mtu yoyote mwenye afya mwanamke au mwanaume na mwenye umri kuanzia miaka 18 ajitokeze kuchangie damu.
Alisema uchangiaji wa damu kwa hiari una faida kwa mtoaji kwa vile napunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kuwepo kwa madini chuma mengi kupita kiasi katika damu kunakodhoofisha utendaji kazi na kuchangia damu mara kwa mara hurekebisha madini  chuma ya ziada  katika mfumo wa damu.
Alisema faida nyingine ni upimaji wa afya pasipo gharama kwa sababu  wakati unapochangia damu mtaalamu wa tiba daktari au muuguzi atapima shinikizo la damu yako, mapigo ya moyo na kukufanyia vipimo vya afya bure.
 
Alisema kutoa damu kunaongeza utambuzi wa kiwango cha chembe hai nyekundu na chembe na huchochea uzalishaji wa seli damu mpya na kuwaomba wanahabari kuendelea kuhamasisha na kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara kwani ni damu ya mwanadamu pekee inayotumika kumuongezea mgonjwa anayehitaji damu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...