Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 8, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SABA YA SIKU YA MLIPAKODI, JIJINI DAR


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti na zawadi, mshindi wa kwanza kwa kulipa kodi, Meneje wa Huduma za Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alois Qande Maleck, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti na zawadi, mshindi wa pili kwa kulipa kodi,Mwakilishi wa Kampuni ya Sigara Tanzania, Paul Makanza, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
 Mshana akipokea Tuzo na Cheti kwa niaba ya Jukwaa la Wahariri.
 Baadhi ya wananchi na walipakodi waliohudhuria sherehe hizo wakimsikiliza Makamu wa Rais.
 Baadhi ya wananchi na walipakodi waliohudhuria sherehe hizo wakimsikiliza Makamu wa Rais.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Polisi, akipokea tuzo na Cheti.......
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi Tuzo na Cheti, Mwananchi Shujaa wa Kodi, Dkt. Shumba, aliyediriki kuwekwa ndani kwa kudai Risiti ya malipo yake ya chumba cha Hoteli katika moja ya hotel katika mikoa ya Tanzania Bara, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi zawadi na Cheti, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila, Ally Mshana, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo. Picha Zote na OMR

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...