Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 4, 2012

KAMPUNI YA SIMU YA MKONONI ZANTEL YATOA OFA MSIMU SABASABA


 (NA PHILEMONI SOLOMON WA FULLSHANGWE)
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya ZANTEL katika msimu huu wa sikukuu ya sabasaba
imetoa ofa maalum ya kifurushi cha Intaneti cha unlimited ambapo mteja anaponunua
anapewa bure kwa siku tatu.
Kauli hiyo ilitolewa Jijini Dar es Salama jana na Mratibu wa masoko wa zantel Nderingo Materu katika viwanja vya maonesho ya 36 ya biashara ya
kimataifa ndani ya uwanja wa Mwalimu JK Nyrere.
Materu alisema sambamba na ofa hiyo pia wateja wasisahau kwamba ukiwa na laini
ya Zantel unaweza kupiga simu kwa dakika moja kwenda mitandao yoyote
nchini.
Hivyo aliwaomba wateja waweze kujipatia laini hizo mapema ambazo zinatolewa bure katika viwanja hivyo kwa watu wote.
Pia alisema zantel ikiwa ni wazamini wa Bongo Star Search kwa mwaka huu imejipanga kisawa sawa kuwainua vijana kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...