|
Wachezaji wa Azam wakiwa wamembeba shujaa wao wa leo Malika Ndeule |
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
AZAM
FC imeingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu, baada ya kuifunga
Simba SC kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2 ndani ya
dakika 120 usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Hadi
mapumziko, Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na
kiungo Mkenya, Humphrey Mieno dakika ya 10, akiunganisha kwa kichwa kona
maridadi iliyochongwa na kiungo mzalendo, Ibrahim Mwaipopo.
Azam ilishambulia zaidi baada ya bao hilo, kabla ya Simba kuzinduka dakika tatu baadaye na kuanza kushambulia pia.
Mchezo
huo ulisimama kwa dakika tano kuanzia ya 14 hadi 19 kutokana na umeme
kukatika uwanjani hapo, hali iliyolazimisha kuwashwa kwa Jenereta.
Kipindi
cha pili Simba walibadilika mno kiuchezaji na kuanza kutawala mchezo
jambo ambalo liliwasaidia kupata bao la kusawazisha dakika ya 78, ambalo
lilifungwa na Rashid Ismail.
Simba
ilipoteza nafasi mbili za wazi za kufunga mabao ndani ya dakika 45 za
kipindi cha pili na mchezo ukamalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao
1-1.
Katika dakika 30 za nyongeza, Simba walifanikiwa kupata bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 110, mfungaji Miraj Madenge.
Azam
walionekana kupagawa baada ya kupigwa bao la pili na kuanza kucheza
rafu za ovyo na kutoa maneno machafu kwa refa, jambo ambalo liliwaponza
kupoteza wachezaji wawili ndani ya dakika mbili.
Refa Waziri Shekha alianza kumtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo Mwaipopo dakika ya 114 na baadaye Jabir Aziz dakika ya 116.
Wakati
refa huyo akijiandaa kupuliza kipyenga cha kuhitimisha mchezo na
mashabiki wa Simba wakiwa wameuteka Uwanja wa Amaan kwa shangwe zao,
beki Emily Mgeta alimuangusha kwenye eneo la hatari beki Malika Ndeule
na hivyo kuwa adhabu ya penalti.
|
Malika amebebwa juu juu |
Beki
Mkenya, Joackins Atudo ambaye amekuwa akipewa dhamana ya kupiga penalti
kwa sasa Azam FC, alikwenda kupiga mkwaju huo na kuukwamisha nyavuni
kuwapatia Watoto wa Bakhresa bao la kusawazisha.
Kutoka
hapo, mchezo ulihamia kwenye mikwaju ya penalti na usiku huu bahati
haikuwa yake kiungo matata chipukizi wa Simba, Haroun Athumani Chanongo,
kwani pamoja na kupiga penalti nzuri iliyokuwa ya pili kwa timu yake,
iligonga mwamba wa juu katikati na kudunda chini kisha kurejea uwanjani.
Wachezaji
wa Simba waliofunga penalti zao leo ni Komabil Keita ya kwanza, Jonas
Mkude ya tatu, Miraj Adam ya nne na Ramadhani Mkiparamoto ya tano,
wakati wa Azam waliofunga ni Gaudence Mwaikimba ya kwanza, Himid Mao ya
pili, Atudo ya tatu, Samir Hajji Nuhu ya nne na Malika Ndeule ya tano.
Kwa matokeo hayo sasa, Azam itamenyana na mshindi wa kesho kati ya Tusker na Miembeni katika fainali Jumamosi.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; William Mweta, Miraj Adam,
Paul Ngalema, Hassan Khatibu/Hassan Isihaka dk89, Komabil Keita, Jonas
Mkude, Ramadhani Singano/Miraj Madenge dk71, Abdallah Seseme/Said Demla
dk 61, Rashid Ismail, Marcel Kaheza/Ramadhan Mkipalamoto dk72 na Haroun
Chanongo.
Azam
FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins
Atudo, Kipre Balou, Seif Abdallah/Gaudence Mwaikimba dk69, Ibrahim
Mwaipopo, Brian Umony/Malika Ndeule dk104, Humphrey Mieno/Jabir Aziz
dk79 na Uhuru Suleiman.
Habari Picha zote na Bongostaz Blog
|
Mgeni
rasmi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho
akisalimiana na kipa wa Azam FC, Mwadini Ally katika mchezo wa leo wa
Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa
Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2
ndani ya dakika 120.
|
|
Kikosi cha Simba leo |
|
Kikosi cha Azam leo |
|
No comments:
Post a Comment