Yondan |
Na Baraka Kizuguto, Antalya
WACHEZAJI Frank
Domayo na Kelvin Yondani waliokuwa wameondoka jana jioni kuelekea nchini
Ethiopia wameshindwa kuungana na wachezaji wenzao wa timu ya Taifa ya Tanzania
Taifa Stars baada ya jana jioni kufika Istambul
kukuta tiketi zao za kwenda Addis Ababa ni za tarehe 09 Februari
2013 hali iliyopelekea kukwama Istambul
na kuamua kurejea mjini Antalya kuungana na wachezaji wenzao waliopo kambi.
Kikosi cha
wachezaji 27 waliopo kambi mjini Antalya kimeendelea na mazoezi ya asubuhi
kujiandaa na mchezo huo wa kesho amabao utakua ni mchezo wa mwisho kabla ya
timu ya Young Africans kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania siku ya
jumapili.
No comments:
Post a Comment