Mkurugenzi wa Maendeleo na Utamaduni
wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka (mwenye suti nyeusi) akimfariji
Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko alipofika nyumbani kwa
marehemu kuhani msiba huo Tabata Bima jijini Dar. (Picha zote na Mo
Blog).
Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo
wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka akitia saini kitabu cha
maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar leo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso akitia saini kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Sajuki.
Msanii mkongwe katika tasnia ya
muziki wa Dansi na Rhumba Kikumba Mwanza Mpango almaarufu kama King Kiki
akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata
Bima jijini Dar leo.
Mzee King Kiki akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari Bw. Herman
Mwasoka (katikati) nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar leo. Kulia ni
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso
Wasanii mbalimbali na wakiendelea
kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Pichani ni Msanii wa muziki Dokii (kushoto) sambamba na Mshiriki wa
Shindano la Big Brother Africa Mwisho Mwampamba na wasanii wengine.
Mchekeshaji maarufu wa The comedy
Masanja Mkandamizi akijifuta jasho kwa mbali akielekea msibani nyumbani
kwa Marehemu Sajuki. Masanja alikuwa ni mmoja wa wahamishaji katika
kuchangia pesa za matibabu ya marehemu Sajuki kwenda nchini India
kupitia kipindi cha Luninga cha The Comedy kinachorushwa na Televisheni
ya TBC.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye huzuni kutafakari kifo cha Sajuki.
VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWASILI:
Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu kushoto) akiwa
ameambatana na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh.Iddi Azzan wakipokelewa
na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba na
wasanii wengine wa filamu baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki
kwa ajili ya kuhani msiba huo.
Mkuu wa Itifaki Bw. Simon Simalenga
wa Clouds Media akimuongoza Mh.Makongoro Mahanga sehemu maalum kwa ajili
ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es
Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro
Mahanga akitia saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu
Sajuki.
Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan naye aliangusha saini kwenye kitabu hicho.
Mzee King Kiki akizungumza jambo na Waheshimiwa Wabunge kwenye msiba wa Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Waheshimiwa wakielekea nyumba ya
jirani walikokusanyika baadhi ya waombolezaji na wasanii wa filamu
nchini kwa ajili ya kuzungumza machache na kutoa Ubani.
Katibu wa Fedha msibani hapo
mchekeshaji maarufu Steve Nyerere akiwakaribisha waheshimiwa wabunge
kuzungumza na hadhira ya waombolezaji (hawapo pichani).
Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es
Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro
Mahanga akitoa salamu zake za rambimbi na kuahidi kuchangia shilingi
200,000/= kwa ajili ya kufanikisha shughuli za mazishi ya mpendwa wetu
Marehemu Sajuki atakayezikwa Kesho Ijumaa katika Makaburi ya Kisutu
jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Iddi
Azzani akielezea kwa majonzi alivyopokea taarifa za msiba wa Sajuki na
kuahidi kushirikiana bega kwa bega na Wastara panapomajaliwa ya Mola
katika malezi ya mtoto aliyeachwa na marehemu na kuwaasa wadau, ndugu,
jamaa na marafiki kumsaidia Wastara kutokana na hali yake na amechangia
kiasi cha Shilingi 500,000= kufanikisha shughuli za mazishi ya marehemu
Sajuki.
Pichani Juu na Chini ni Umati wa
waombolezaji ukisikiliza nasaha za waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani)
walipofika nyumbani kwa marehemu Sajuki kuhani msiba huo.
Kazi ya kuosha vyombo si kina Dada
tu, hata kina Kaka wanaweza pia....Pichani ni baadhi ya Watangazaji wa
Clouds Radio wakiongozwa na Dina Marios kushiriki kuosha vyombo
vilivyotumika katika msiba huo huku wakisaidiana na waombolezaji
wengine.
Mganga wa Jadi anayefahamika kwa jina
la Dokta Manyaunyau (kushoto) sambamba na Msanii wa filamu nchini Cloud
wakisikiliza mawaidha ya waheshimiwa wabunge (hawapo pichani).
Mkuu wa Itifaki msibani hapo Bw.
Simon Simalenga wa Clouds Media akimpokea Mwenyekiti wa kamati ya
Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete
alipowasili nyumbani kwa marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani maeneo ya
Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu
ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa pole
baada ya kusaili kwa baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Sajuki
msibani hapo.
Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na
Baba mzazi wa marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko nyumbani kwa marehemu
Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu
ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitia saini
kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki leo.
Bw. Ridhiwani Kikwete akimpa maneno ya faraja Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko.
Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa mkono wa pole kwa mke wa marehemu Sajuki Bi. Wastara (mwenye buibui).
Bw. Ridhiwani Kikwete akimfariji mama mzazi wa Marehemu Sajuki alipofika nyumbani hapo kuhani msiba huo.
Katibu wa fedha msibani hapo Steve Nyerere akitetea jambo na Bw. Ridhiwani Kikwete.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini
(TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha
Bw. Ridhiwani Kikwete kuzungumza machache na waombolezaji.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu
ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akizungumzia
marehemu Sajuki na kuwataka wanawake kuiga mfano wa Maisha ya Sajuki na
Wastara jinsi walivyokuwa wakiishi na Upendo mpaka Umauti ulipomkuta
marehemu Sajuki na kuwasisitiza kuenzi yale yote mema aliyokuwa akifanya
kipindi cha uhai wake na kuwamasisha Umoja na Mshikamano baina yao. Bw.
Ridhiwani Kikwete naye alichangia Shilingi 500,000/= kwa ajili ya
kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu Sajuki anayetarajiwa kuzikwa Kesho
Ijumaa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani).
Marehemu Sajuki alikuwa kipenzi cha
watoto na wakubwa pia. Pichani ni Umati wa watoto wanaokaa jirani na
Nyumba ya Marehemu Sajuki wakiwa wamekusanyika huku wakionyesha majonzi
na simanzi tele.
No comments:
Post a Comment