Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 30, 2014

KINANA AKERWA VIONGOZI KUPORA ARDHI YA WANNCHI


 Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza maswali na kuhusu kero mbalimbali walizonazo wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara kwenye mkutano wa hadhara. uliofanyika jana katika kata hiyo.
 Baada ya kusikiliza maswali mengi yakihusiha kero ya wananchi kuporwa ardhi na baadhi ya viongozi kwa kushirikiana na  baadhi ya wawekezaji, Kinana alionekana kukerwa kwa kiasi kikubwa na kadhia hiyo na kuahidi  suala hilo kwenye vikao vya ngazi ya juu vya chama kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

 Kinana alisikitishwa zaidi  baada ya kuonekana kwamba viongozi na wawekezaji wamekuwa wakitumia vyombo vya sheria ikiwemo mahakama kukandamiza haki za wananchi hao kwa kuwa wengi wao hawajui taratibu za vyombo vya sheria hata kama wana haki za msingi.
Kufuatia kero hiyo na nyingine zilizoulizwa na wananchi kwenye mikutano kwa nhyakati mbalimbali, Kinana ameahidi kuwaripoti kwa Rais Jakaya Kikwete viongozi ambao wamekuwa chanzo cha unzembe na kudumaza haki za wananchi hasa wa maeneo ya vijijini wilayani humo mkoani Manyara
Katika ziara hiyo ya siku saba mkoani Manyara,  Kinana ameambatana na Katibu wa NEC,  Itikadi  na Uenezi,  Nape Nnauye,  kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
 Baadhi ya Wanahabari walioko kwenye msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana wakiwa kazini.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
 Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
 Wananchi wa kata ya Ayamango na mabango yao.
 Wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Ayamongo,Babati Vijijini mkoani Manyara
 Katibu wa NEC Itikadi,Sisa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia  Wananchi wa kata ya Ayamango (Gallapo),Wilayani Babati Vijijini mkoani Manyara alipokwenda kuzindua shina la Wakereketwa,kutoa kadi kwa wanachama wapya sambamba na kufanya mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini,Mh.Jitu Son na viongozi mbalimbali wachama wa Wilaya na Mkoa,wakikagua moja ya jengo la mradi wa ujenzi wa chuo cha Ualimu cha Sayansi Mamire,wilayani Babati vijijini mkoani Manyara.

PICHA NA MICHUZIJR-BABATI VIJIJINI- MANYARA. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...