Miss Sinza 2013 Prisca Clement katikati mara baada ya kushinda taji la vipaji katika mashindano ya Miss Tanzania 2013
======= ====== ======
Waandaaji
wa mashindano ya kumsaka mrembo wa Sinza, Miss 2014 wametoa wito kwa
wasichana wenye vigezo vya kuwania taji la mwaka huu kujitokeza katika
mazoezi yanayoendelea kwenye ukumbi wa Meeda Club uliopo katika barabara
ya Sinza Mori na Lufungila jijini.
Akizungumza
jijini jana, Muandaaji wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa
lengo lao ni kuwa na warembo wengi ili kuwapa nafasi majaji kuchagua
washindi ambao wataiwakilisha vyema Sinza na vitongoji vyake katika
mashindano ya Kanda ya Kinondoni na Miss Tanzania.
Majuto
alisema kuwa mpaka sasa jumla ya warembo nane wamejitokeza katika
mazoezi ya mwaka huu, idadi ambao haitoshi kutokana na malengo yao
ambayo ni warembo 20.
Alisema
kuwa uwepo wa washindani wengi, kunatoa changamoto hata kwa majaji na
kutoa mrembo bora zaidi na kuwa mwakilishi wa kweli. “Hatujafunga
milango ya kuwapokea warembo, tunawaomba wafike mazoezini kuanzia saa
10.30 jioni na kukutana na wakufunzi wetu, Fomu zinatolewa bure,”
alisema Majuto. Majuto
pia aliwaomba wadau wa mashindano ya urembo nchini kujitokeza kudhamini
mashindano hayo kwa lengo la kuleta maendeleo, kuongeza ushindano mbali
ya kutangaza biashara zao.
Alisema
kuwa ni fursa pekee kudhamini mashindano hayo kutokana na mvuto uliopo,
kwani watazamaji wengi ufika kuangalia mazoezi na wakati wa mashindano.
Taji
la Miss Sinza linashikiliwa na Miss Tanzania, Prisca Clement alimaliza
katika hatua ya 10 bora katika mashindano ya mwaka jana ya Miss Tanzania
na pia alishinda taji la mrembo mwenye kipaji katika mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment