Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 24, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA KUKAMUA MAFUTA YA UFUTA CHA TAKEMOTO, NAGOYA JAPAN



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona 
(wa pili kushoto) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakiongozana 
wakati walipokuwa wakielekea kutembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo Japan, jana Mei 22, 2014, 
akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini Japan.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal na ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu kiwanda hicho kinavyofanya kazi 
hadi kupatikana mafuta ya Ufuta, wakati walipofika kiwandani hapo kujionea kutembelea na kujionea shughuli za uzalishaji, jana Mei 22, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta 
cha Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyoanza kuandaliwa kuelekea katika mashine za kukamua mafuta. Hapa ni hatua ya kwanza zinaposhushwa mbegu hizo na kuingia moja kwa moja kwenye mitambo.
  akiendelea kupata maelezo....

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha Mafuta ya Ufuta cha 
Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyosafiri hadi kufika katika Kinu cha kuzisaga hadi kupatikana mafuta hayo, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan, jana
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakionyeshwa mbegu za ufuta na Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakionyeshwa mafuta ya ufuta na Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya hayo cha Takemoto, Akira Ogawa, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan, jana

 Wakiendelea kutembelea kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...