Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mtandao wa Teknolojia ya kisasa ya China
{ Huawei Techonogies } Nchini Tanzania Bwana Bruce Zhang hapo Ofisini
kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Huawei Technologies Nchini Tanzania Bwana Bruce
Zhang akimuonyesha Balozi Seif mpango kazi wa Kampuni yake katika mfumo
wa teknolojia ya kisasa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kulia akiwa katika picha ya
pamoja na Uongozi wa juu wa Kampuni ya Huawei Technologies Nchini
Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Bwana Bruce Zhang
aliyepo kati kati yao .Kulia yao ni Mwakilishi wa Huawei Technologies Ofisi ya Zanzibar Bwana Peter Jiang.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Huawei Technologies Nchini Tanzania Bwana Bruce
Zhang akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Nyuma yake aliyevaa shati nyeupe ni Mwakilishi wa Huawei Technologies Ofisi ya Zanzibar Bwana Peter Jiang.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*******************************
Kampuni
ya Kimataifa ya mawasiliano ya Teknolojia kutoka Nchini Jamuhuri ya
Watu wa China ya Huawei Technology ambayo tayari imeshafungua tawi lake
Mjini Dar es salaam imeonyesha nia ya kutaka kusaidia Zanzibar
kimaendeleo katika mfumo wa kisasa wa Teknolojia.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni hiyo Nchini Tanzania Bwana Bruce Zhang alitoa kauli
hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Sei Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana
Bruce alisema Kampuni ya Huawei Technologies ambayo imepanga kutumia
kiasi cha Dolla Bilioni Tano { U$ 5,000,000,000 } ndani ya kipindi cha
miaka mitano katika kutekeleza miradi ya mafunzo ya Teknolojia, fursa
za masomo ya nje na Afya ikilenga zaidi kwa wananchi wakipato cha
kawaida.
Alisema
mafunzo ya Teknolojia ya kisasa tayari yameshaanza kutolewa na Taasisi
hiyo kwa kuwapatia watendaji wa makampuni yanayotoa huduma za simu
sambamba na wanafunzi maskulini ili kuwajengea uwezo wa kazi kupitia
mfumo wa kisasa wa mawasiliano.
Alieleza
kwamba miradi kadhaa ya kielimu imeanzishwa na taasisi hiyo kuwapatia
mafunzo wanafunzi wa vyuo na skuli mbali mbali nchini Tanzania zikiwemo
fursa za nje ya nchi pamoja na kutafuta wanafunzi wenye vipaji maalum
watakaowezeshwa kujengewa uwezo zaidi wa kielimu.
“
Tumekuwa na utaratibu wa kila mwaka ndani ya Kampuni yetu kutenga
bajeti maalum kwa ajili ya mafunzo kwa wafanyakazi wa taasisi za
mitandao, wanafunzi, utoaji wa vifaa kama Kompyuta pamoja na misaada
katika sekta ya afya “. Alifafanua Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kampuni ya
Huawei Technologies.
Aidha
Bwana Bruce Zhang alifahamisha kwamba Kampuni yake kwa kushirikiana na
taasisi za Teknolojia ya mawasiliano zimekuwa zikiendesha shindano la
kutafuta mabingwa wa mitandao ya Kompyuta { ITC – Star } ili kuzalisha
wataalamu zaidi katika fani hiyo muhimu hivi sasa.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliueleza ujumbe huo wa Kampuni ya Huawei Technologies kwamba Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa iko katika kipindi cha mpito
ikijiandaa na mfumo wa matumizi ya Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano {
E Government } katika utendaji wa Wizara zake zote.
Balozi
Seif aliutaka uongozi wa Kampuni hiyo kujitayarisha na maombi ya miradi
itakayoweza kuwekeza na taasisi hiyo hapa Zanzibar ili kwenda sambamba
na Serikali katika mfumo wa matumizi hayo ya teknolojia ya kisasa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi wa Huawei
Technologies kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa kila msaada
ili kuona malengo la Kampuni hiyo yanafaidisha pande zote mbili.
No comments:
Post a Comment