Kamanda
wa Polisi Kinondoni akiongea na waandishi wa habari kuelezea ni jinsi
gani watashughulikia shida ya barabara hiyo ya kutoka kituoni makumbusho
kuelekea mwenge
Kondakta
wa Daladala akiwa ameumia mkono wake wa kulia baada ya kukatwa na side
mirror ya basi la UDA alipokuwa akilizuia lisipakie abiria na kuondoka
kwenda mwenge
Hapo
ni Madereva na makondakta wakilikimbiza basi la UDA ambalo lilimkata
mkono dereva mwenzao wakati wanalizuia lisiweze kutoka ndani ya kituo
kuendelea na safari.
Hili
ni moja ya basi la abiria likiwa limewekea magogo ili lisiweze
kuendelea na safari kuelekea mwenge Bali kuishia kituo cha makumbusho na
kuweza kushiriki mgomo huo
Daladala zikiwa zimepaki na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea Mwenge
Daladala zikiwa ndani ya kituo cha makumbusho zimepaki baada ya mgomo wao wa leo mchana
Msururu wa daladala zikiwa ndani ya kituo cha makumbusho baada ya kugoma leo kuelekea mwenge kupeleka abiria
Polisi wakiwa ndani ya kituo cha makumbusho kulinda usalama wa eneo hilo la kituo
Daladala zikiwa zimepaki na kugomakupeleka abiria mwenge
Madereva na Makondakta wakizuia magari mengine kupita na kupeleka abiria
Waandishi
wa Habari wakichukua Maelezo kutoka kwa Afisa wa Polisi Kinondoni
kuhusu mgomo huo wa daladala uliofanywa leo mchana na madereva wa magari
ya Tandika,Mbagala,Buguruni ambayo yanatumia kituo cha Makumbusho
kushusha abiria
Madereva
wa daladala kwa mbaliiii kama wanavyoonekana wakiendelea kuongea na
Viongozi wa Serikali kuhusu Tatizo lao la barabara mbovu ya makumbusho
kuelekea mwenge
Madereva
na Makondakta wa mabasi yanayofanya Safari zake kati ya mbagala,tandika
kupitia kituo cha makumbusho wakijadiliana na viongozi wa sumatra na
polisi Ili kuweza kujua watatoa Suluhisho gani ili kuweza kutatua
tatizo la barabara mbovu eneo la makumbusho
Mkaguzi kutoka Sumatra akiongea na Vyombo vya habari na madereva na makondakta
Afisa
wa Polisi Kinondoni akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari baada ya
kuweza kukubaliana na Madereva na Makondakta kutumia barabara kuu kwa
siku mbili ili wakati wakiendelea kushughulikia utaratibu wa
kutengenezwa kwa barabara za ndani ambazo walikuwa wanapaswa kuzitumia
Abiria
wanaotumia njia ya makumbusho kuelekea Mwenge wakitokea Tandika na
Mbagala leo wameonja Joto ya jiwe kwa takribani masaa manne baada ya
mabasi yanayoptumia kituo cha ndani kugoma kupeleka abiria mwenge
kutokana na ubovu wa barabara za ndani wanazotumia kupita kuelekea kituo
cha mwenge.
Sakata
hilo lilianza pale magari yalipofika kituo cha ndani cha makumbusho na
kuwashusha abiria wote na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea Mwenge,
ndipo mzozo mkubwa ulipozuka na kupelekea Sumatra na vyombo vya Usalama
kufika eneo la tukio na kuweza kuongea na madereva hao, lakini madereva
hao na makondakta waliendelea kugoma mpaka pale walipoahidiwa kuwa
ndani ya wiki moja barabara hizo zitakuwa zimerekebishwa na kuwa
nzuri,hivyo watumie njia kuu kuelekea Mwenge.
PICHA NA HABARI NA DJ SEK BLOG
No comments:
Post a Comment