Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 25, 2014

MATUKIO YA MKUTANO WA (AFDB) RWANDA



 Katibu Mkuu Dkt.Servacius Likwelile akiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu katika Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ecobank Jijini Kigali Rwanda.
 Waziri wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkuatno mkuu wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika uliofanyika Kigali Nchini Rwanda.
Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akijadiliana jambo na mmoja wa washiriki wa Mkutano wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unafanyika Kigali Rwanda. Pembeni ni mwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na msaidizi wa Waziri Bw.Thomas Mabeba.

Mkutano Mkuu wa 49 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika umemalizika Jijini Kigali,Rwanda kwa Viongozi wa Benki kuahidi kujenga Afrika ambayo ni itakuwa na Umoja,mshikamano na yenye miundombinu ya uhakika.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika,Dkt. Donald Kaberuka amesema Benki itasaidia utekelezaji wa mipango bora ambayo itatokana na majadiliano yatakayofikiwa kwenye vikao nchi wananchama. Miongoni mwa vipaumbele vya benki kwa kipindi cha miaka kumi ijayo ni kujenga mazingira ya kuwa na uchumi imara na endelevu,usimamizi wa maliasili za bara la Afrika na ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha zaidi wanawake na vijana katika ukuaji wa uchumi wa bara la Afrika.
Katika kuhakikisha maendeleo ya Bara la Afrika yanafikiwa kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kipindi cha miaka 50 ijayo ni  pamoka na kusimamia utekelezaji wa mpango wa ‘Afrika 50’ ambao utapelekea kuongeza ufadhili wa kiasi cha Dola bilioni 100 ambazo zinahitajika katika kuimarisha miundombinu ya Bara la Afrika.
Awali katika mkutano uliofanyika kati ya Mkurugenzi wa AfDB kanda ya Afrika Mashariki Nd. Gabriel Negatu na ujumbe wa Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile aliishukuru benki kwa jitihada zake za kuhakikisha Tanzania inatekeleza kwa ufanisi miradi yote inayofadhiliwa na Benki hiyo. ‘Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika ambayo inanufaika na fedha kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika,kwa sasa tuna zaidi ya miradi 31 ambayo inatekelezwa na AfDB’ alisema Dkt.Likwilile.
Mwishoni mwa Mkutano wa Magavana wa Benki,Pia walipitisha kuanzishwa kwa ‘Africa Growing Together Fund (AGTF)’,na kiasi cha dola bilioni 2 zitatolewa na china ili kuwezesha AfDB kukabiliana na kuongezeka kwa mahitaji ya kikanda kwa nchi wanachama wa benki na wateja wa sekta binafsi.
Mkutano ujao wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika utafanyika Jijini Abidjan,nchini Ivory coast ambayo pia itakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 50 ya benki ya maendeleo ya Afrika yatakayoadhimishwa Novemba,2015.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...