Mbunge wa jimbo la Singida Mjini, Mh.
Mohammed Dewji (MO), akizungumza na waumini wa Msikiti wa kijiji cha
Mtamaa wakati wa ziara yake ya siku tatu jimbo kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gulam Dewji amewahimiza
waumini wa madhahebu mbalimbali ya dini kuendelea kushirikiana na
serikali ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo endelevu.
Mbunge Dewji maarufu kwa jina la MO,ametoa wito huo hivi karibuni kwa
nyakati tofauti wakati akikagua ujenzi wa misikiti na makanisa jimboni
kwake.
Amesema madhehebu ya dini mbalimbali yana mchango mkubwa sana katika
kusukuma gurudumu la maendeleo,kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa
ujumla.
Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.
"Mchango wa madhehebu ya dini unasaidia mno kuendeleza amani na
utulivu kuanzia ngazi ya kaya,kijiji hadi taifa.Amani na utulivu uliopo
hivi sasa ndio unaotusaidia tumwabudu Mungu kwa uhuru na pia kujiletea
maendeleo bila vikwazo",amesema.
Dewji amesema ili kuonyesha imani yake kubwa kwa madhehebu ya dini
safari hii ameamua kukagua ujenzi wa makanisa na misikiti ya jimboni
kwake ili aweze kuyaunga mkono katika ujenzi huo unaoendelea.
"Ninyi ni mashahidi wangu wazuri juu ya maendeleo ya sekta mbalimbali
tuliyoyapata jimboni mwetu kwa kushirikiana mimi na ninyi.Baada ya
kufanya makubwa kwenye sekta ya elimu,afya,barabara na maji,sasa
nimeamua kwa moyo wangu wote kuboresha ustawi wa madhehebu ya
dini",amesema.
Akifafanua zaidi, amesema kupitia kwa katibu mkuu wa CCM
taifa,anatarajia kukabidhi misaada ya mabati na mifuko ya saruji yenye
thamani ya zaidi ya shilingi 127 milioni kwa misikiti 51 na makanisa 30.
No comments:
Post a Comment