Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 5, 2014

KAMPUNI YA PR PROMOTION YATAMBULISHA MISS REDDS MBAGALA 2014.


 Afisa Habari Kampuni ya PR Promotion Bw. Victor Mkumbo (kushoto) akitoa maelezo mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu utambulisho wa Miss Redds kwa Kitongoji cha Mbagala kwa mwaka 2014. Katikati ni Mratibu wa Kampuni hiyo Bw. Tesha Japhet na kulia ni Meneja wa Kampuni ya PR Promotion Bw. Gervas Sinsakala.
 Baadhi ya warembo watakaoshirki kinyang’anyiro hiko wakiwa wamepozi wakati wa utambulisho wao katika Mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari walioshiriki katika Mkutano wakisikiliza na kupiga picha mbalimbali kuhusu utambulisho wa Miss Redds kwa Kitongoji cha Mbagala kwa mwaka 2014.
****************************************************
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
KAMPUNI ya PR Promotion inatarajia kuleta kitongoji kipya katika mashindano ya Urembo Tanzania kupitia Wilaya ya Temeke ambayo ni Miss Mbagala kwa mwaka 2014.
Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa Kampuni hiyo Bw. Tesha Japhet wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam uliohusu tambulisho wa Miss Redds Mbagala kwa mwaka 2014.
“Hii ni mara ya kwanza kitongoji cha Mbagala kuandaa mashindano ya Miss Tanzania baada ya kuongezwa na Kamati ya Redds Miss Tanzania mwaka huu, hivyo wilaya ya Temeke itakuwa na vitongoji vine ambavyo ni Chango’mbe, Kurasini, Kigamboni na Mbagala”. Alisema Japhet.
Bw. Japhet ameongeza kuwa washindi watatu wa mwanzo katika mashindano hayo watashiriki moja kwa moja katika mashindano ya Miss Redds Temeke 2014.

Mashindano hayo ya Miss Mbagala 2014 yatajumuisha jumla ya washiriki 16 kutoka maeneo mbalimbali ya Mbagala na majina yao ni Amina Salim (20), Aquilina Paul (22), Restuta Charles (21), Suzan Paul (19), Natalia Rohath (22), Grace John (20), Neema Roman (19), Lucrecia Mushi (20), Subira Ally (23), Lucy Lyombo (20), Joyce Mkandila (20), Lulu Baraka (22), Macklina Robert (21), Sylivia Robert (24), Esther Mnahi (20) na Maureen Msangi (20).

Aidha, Warembo wote watatambulishwa rasmi siku ya Ijumaa ya tarehe 9 Mei, 2014 sambamba na uzinduzi rasmi wa Miss Mbagala 2014 utafanyika katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 2 usiku.
PR Promotion ni Kampuni ya burudani iliyosajiriwa na BASATA tangu mwaka 2009 imekuwa ikifanya maonesho mbalimbali ya sanaa ikiwemo urembo pamoja na kuendesha mikutano na waandishi wa habari na inajihusisha na upigaji picha za mnato na video katika matukio mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...