Kibao
kikionesha eneo la Hifadhi ya Mazingira ya Asili ya Chome Shengena Wilaya ya Same
Mkoa wa Kilimanjaro.
|
Sehemu ya Msitu wa Chome ambayo ilichomwa Moto na wachimbaji Madini. |
Sehemu ya mpaka ya Msitu wa Chome na zilizokuwa na zisizokuwa za Msitu wa Hifadhi upande wa kulia. |
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MALIASILI NA UTALII
WAKALA
WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA
TAARIFA
YA HIFADHI YA
MAZINGIRA ASILI CHOME
UTANGULIZI.
Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia wa Chome (Shengena) ni
msitu wa Serikali Kuu unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
Msitu huu ulitangazwa kwa mara ya kwanza
kuwa Msitu wa Hifadhi mwaka 1951 kwa tangazo la Serikali Na. 125 la tarehe
25/05/1951. Ikafuatiwa na tamko la marekebisho kwa tangazo la Serikal Na 303 la
tarehe 20/06/1958.
Hifadhi hii ina ukubwa wa eneo la Ha 14,283 na
urefu wa mpaka wa Km 67. Hifadhi inazungukwa na vijiji 27 vilivyoko
katika kata 11.
Katika kuhakikisha kuna usimamizi mzuri Msitu huu
umegawanyika katika safu tano za usimamizi ambazo ni Chome, Suji, Mamba
miyamba, Bombo na Mbaga.
MALENGO
Kutokana na mpago kazi wake hifadhi hii ina malengo
yafuatayo:
1 Kutunza mazingira asili, mfumo wa ikologia katika uasilia
wake.
2 Kuimarisha uhifadhi wa baianowai na mtawanyiko wake.
3 Kuimarisha mfumo wa ekolojia.
4 Kulinda mmomonyoko wa udongo na maporomoko ya ardhi na
miamba.
5 Kuimarisha mafunzo na tafiti mbalimbali.
6 Kushirikisha jamii na wadau wote katika kulinda, kuhifadhi
na kuendeleza uhifadhi.
7 Kuelimsha jamii inyozunguka hifadhi njia mbadala ya
kupunguza umaskini.
HALI YA AWALI YA HIFADHI
Hali ya Msitu huu ilikuwa na chnagamoto kubwa za uhifadhi
ambazo ni kama zifuatavyo;-
• Uchimbaji wa madini
ndani ya hifadhi
• Uchomaji moto
• Upasuaji wa mbao
• Uchungiji wa mifugo
• Ushiriki mdogo wa
wananchi katika kulinda hifadhi hii.
KUPADISHWA HADHI KUWA YA MAZINGIRA ASILIA
Kuna sababu nyingi za kimsingi
na za kitaalam zilizopelekea serikali kupandisha hadhi ya uhifadhi wa misitu
huo kuwa hifadhi ya mazingira asilia.
SABABU HIZO NI KAMA IFUATAVYO:-
•Iligundulika kuwa eneo hili lina bio-anuwai nyingi za mimea na wanyama
ambao ni adimu, ndwele na wanaopatikana eneo hili tu.
• Eneo hili linatunza maumbile ya asili na kuboresha hali ya hewa na
kuhifadhi gesi ukaa kuvuta mawingu yanayoleta mvua za mara kwa mara.
• Ni tanki la maji kwa wakazi wanaozunguka hifadhi hii.
• Ni kivutio kwa watalii na hivyo utalii wa ekolojia unaendelezwa.
• Ni sehemu maalum kwa tafiti za ekolojia ya misitu ya tropiki.
HALI YA HIFADHI BAADA KUPANDISHWA HADHI
Hatua hii ya kuupandisha Msitu na kuwa Hifadhi ya mazingira
asili kwa kiasi kikubwa imepunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zilizokuwa
zinaikabili hifadhi hii ambapo shughuli za uchimbaji wa madini
zimepungua,kutoka watu zaidi ya 40 kwa siku na kuwa na wastani wa mtu mmoja
hadi 4 kwa siku.matukio ya moto yamepungua pamoja na mifugo. Wananchi wameelewa
umuhimu wa utunzaji wa hifadhi.
Ili kuhakikisha kuwa uhifadhi unaendelea na hatimaye kufikia
malengo tajwa hapo juu hifadhi hii inafanya shuguli zifuatazo;
•Kufanya Doria
shirikishi ndani na nje ya Hifadhi kwa kushirikiana na kamati za maliasili za
vijiji
• Kuimarisha mpaka wa
hifadhi kwa kusafisha na kupanda miti.
•Kurejesha maeneo
yaliyoharibiwakwa kufukia mashimo yaliyoachwa wazi na wachimbaji madini haramu,
kurudisha mikondo ya maji kwenye njia za asili na kupanda miti
• Kuandaa na kusafisha
njia za kitalii.
•Kuwasaidia wanavijiji
kuanzisha bustani za miti ya asili kwaajili ya kupanda mashambani.
•Kuwawezesha wanavijiji
wanazunguka hifadhi kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiongezea kipato mfano
ufugaji nyuki.
•Kuanzisha Kamati za
Maliasili za vijiji ili kuongeza ushiriki wa jamii zinazozunguka hifadhi hii.
USHIRIKI WA TAASISI NA MASHIRIKA MENGINE KATIKA UHIFADHI
Katika kuhakikisha kuwa hifadhi hii inatekeleza majukumu
yake kikamilifu hifadhi inashirikiana na taasisi na mashirika mbali mbali
kama;-
• Ofisi ya Mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro
• Ofisi ya mkuu wa
wilaya Same
• Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri
ya Wilaya ya Same.
• Ofisi ya mkuu wa kituo
cha polisi Same
• Mfuko wa hifadhi ya
milima ya Tao la mashariki (EAMCEF)
• Shirika la Kuhifadhi
Misitu Tanzania (TFCG)
• Serikali na
halmashauri za vijiji
• Wananchi wanaozunguka
hifadhi
MAFANIKIO
Kwa kushrikiana na wadau wengine pamoja na serikali za
vijiji mafanikio yafuatayo yamepatikana kipindi cha mwaka 2012 – 2014)
•Kwa kufanya doria
shirikishi tumefanikiwa kuwaondoa wachimbaji wa madini ndani ya hifadhi ambao
walikuwa takribani 2000 na kufanikiwa kukamata zana mbalimbali wanazotumia
katika uchimbaji kama mashine za kusukumia maji (water pump) 20 Beleshi 30
Surulu10 n.k
•Upasuaji mbao
umepungua ambapo kutokana na doria hizo misumeno 10 pamoja na wahalifu
walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria pia mazao mbalimbali ya
misitu yalikamatwa ikiwemo milango 160 pamja na mbao vpande 100
• Jumla ya wahalifu 54
walikamatwa 16 kati yao wamehukumiwa vifungo vya kati ya mwaka mmoja hadi
miwili. 29 wamelipa faini 9 kesi zao bado zipo mahakamani.
•Kuuongeza ushiriki wa
wananchi kwa kuanzisha Kamati za Maliasili za vijiji kwa kila kijiji.ambazo
jumla yao ni kamati 27.
•Kuwaondoa wavamizi wa
hifadhi ambao walivamia kwa lengo la kulima au kuweka makazi ndani ya hifadhi.
•Kuimarisha mpaka wa
hifadhi kwa kupanda miti na kuweka mabango ili kuzuia uvamizi wa hifadhi.
• Kuwawezesha wananchi
kuanzisha bustani zao za miti ili kupanda katika mashamba yao.
•Matukio ya moto
yaliyowahi kutokea yamepungua kutoka matukio 5 kwa mwaka hadi tukio moja kwa
siku.
•Idadi ya mifugo
imezidi kupungua kutoka wastani wa ngombe 50 hadi wastani wa ngombe watano
wanaoingia ndani ya
hifadhi.
CHANGAMOTO
•Upungufu wa rutuba
katika mashamba ambao unasababisha jamii kutovuna mazao ya kutosha kukidhi
mahitaji yao.
•Mtandao wa
wafanyabiashara wa mazao ya misitu hasa mbao zinazokamatwa na miti
comphour(mkulo) kwa kutengenezea milango , vitanda n.k.
No comments:
Post a Comment