Msimamizi
wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents, Bw Tony Akwesa akitoa
maelekezo kwa washiriki waliojitokeza kwaajili ya shindano la Tanzania
Movie Talents kwa kanda ya Pwani unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaam
Baadhi
ya washiriki wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuchukua fomu za ushiriki
wa shindano la Tanzania Movie Talents lililoanza rasmi leo Kwa Kanda ya
Pwani.
Washiriki waliojitokeza kuchukua fomu za Shindano la Tanzania Movie Talents wakisoma fomu kwa umakini kabla ya Kujaza
Washiriki wakipewa maelekezo na Mmoja wa wafanyakazi wa Proin Promotions
Washiriki wakisoma fomu kwa makini
Wakielekezwa Kujaza Fomu za ushiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents.
Shindano
la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo Katika Kanda ya Pwani
Ambapo usaili unaendelea kufanyika leo na kesho katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam ambapo takriba washiriki
zaidi ya 250 wameweza kuchukua fomu za ushiriki wa Shindano hilo
Shindano
hili ni muendelezo wa shindano la kusana vipaji vya kuigiza ambalo
limefanyika tayari kwa Kanda Tano za Tanzania yaani Kanda ya Ziwa, Kanda
ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini na Kanda ya
Kaskazini na sasa tunamalizia Kanda ya Pwani ambapo washindi watano
watapatikana kwa Kanda ya Pwani na kila mmoja atajinyakulia kitita cha
Shilingi Laki Tano taslimu.
Shindano hili limelenga kuibua vipaji vilivyojificha ambavyo havikuwahi kupata nafasi ya kuonekana.
Baada
ya Wasindi watano kupatikana kwa Kanda ya Pwani, washindi takribani 20
kutoka kanda zote sita za Tanzania watawekwa katika kambi moja Jijini
Dar Es Salaam na watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu Wa Sanaa kutoka Chuo
Cha Sanaa cha Bagamoyo na baadae kushindanishwa na hatimaye mshindi
mmoja kupatikana na Kuibuka na zawadi nono ya Shilingi Milioni 50 za
Kitanzania.
Vilevile
Washiriki kumi watakaopatikana katika fainali hiyo watakuwa chini ya
Kampuni ya Proin Promotions na watatengeneza filamu ya pamoja na
hatimaye Kuweza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo
No comments:
Post a Comment