Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwasilisha
Bungeni Mjini Dodoma Mei 27,2014 hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa
mwaka wa fedha 2014/2015. Baada ya mjada mrefu ambao pia ulihusisha
mahusiano baina ya Tanzania na nchi jirani na namna Tanzania
inavyosuluhusha migogoro kwa majirani na lile suala la wapiganaji waasi
wa M23 nchini Congo DRC Bajeti hiyo ilipita.
Wakuu
wa Taasisi Mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, wakifuatilia Bunge wakati wa mjadala wa bajeti
ya wizara yao.
Wanafunzi kutoka Vyuo vikuu vya Mzumbe (MU) na Dar es Salaam (UDSM) wakifuatilia mijadala
ya Bunge wakati wakijadili na kupitisha bajeti ya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Maofisa mbalimbali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wakiwa Bungeni mjini Dodoma kufuatilia hotuba ya Bajeti ya
Wizara hiyo Mei 27,2014
No comments:
Post a Comment