Aliyewahi
kuwa mwanamuziki wa dansi wa bendi za African Revolution 'Wana tam tam'
na Double M, enzi hizo chini ya uongozi wa Muumin Mwinjuma, Amina
Ngalum A.K.A Japanese (pichani enzi za uhai wake) amefariki dunia nchini
Thailand, ambako alikuwa akifanya shughuli zake za kimuziki.
Akizungumza
na mtandao huu, mtoaji wa habari hizi, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wake
katika bendi ya Tam Tam, Asha Baraka, amesema kuwa Amina amefariki dunia
wakati akifanyiwa upasuaji.
''Imeelezwa
kuwa Amina alianza kuugua ghafla, huku akilalamika kuwa kichwa
kinamuuna na tumbo, na ndipo alipokwenda hospitali kwa ajili ya kupima
na kuambiwa kua alikuwa na uvimbe kichwani na hivyo kutakiwa kufanyiwa
upasuaji,
Aidha
ilielezwa kuwa uvimbe huo ulikuwa ukitoa damu na baada ya kuanza
kufanyiwa upasuaji hakuweza kuamka tena na ndipo umauti ulipomfika''.
alisema Asha Baraka.
Mpaka
mauti yanamfika, Amina alikuwa mwanamuziki wa bendi ya Jambo Survivors.
Msiba upo Kipunguni B, Machimbo jijini Dar es Salaam. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMINA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
No comments:
Post a Comment