Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mfanyabiashara na mwekezaji
maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote katika uwanja wa ndege wa kiwanda
chake cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400
Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni
Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu Rais
Dkt Jakaya Mrisho kikwete akipata maelezo toka kwa mfanyabiashara na
mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote wakati akizungushwa
kuangalia kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko
kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme wa kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila MajanbuRais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa aina ya mali ghafi inayotumika alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika mfuko wa saruji alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014.PICHA NA IKULU
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kwenye mtambo wa kuzalisha umeme wa kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila MajanbuRais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa na mfanyabiashara na mwekezaji maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014. Kushoto ni Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ishaya Samaila Majanbu
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa aina ya mali ghafi inayotumika alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika mfuko wa saruji alipotembelea kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant kilichoko kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa Lagos alipotembela May 9, 2014.PICHA NA IKULU
. Ni kile kinachomilikiwa na mwekezaji anayejenga kiwanda cha saruji Mtwara
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ametumia siku nzima Ijumaa, Mei 9, 2014, kutembelea kiwanda kikubwa
zaidi cha saruji kuliko kingine chochote duniani cha Dangote Cement
Obajana Plant na kinachomilikiwa na tajiri mkubwa zaidi wa Afrika, Bwana
Aliko Dangote, ambaye pia anajenga kiwanda kikubwa cha saruji mjini
Mtwara.
Akiandamana
na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Abdallah Kigoda, kwa siku
nzima, Rais Kikwete ametembelea kiwanda hicho cha Saruji cha Dangote
kilichoko katika eneo la Obajana, Jimbo la Kogi, kilomita 400 kaskazini
mashariki mwa mji maarufu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos.
Rais
Kikwete ambaye alikuwa nchini Nigeria kuhudhuria Kongamano ya Uchumi
Duniani-Afrika (WEFA) mwaka huu aliamua kutumia siku yake ya mwisho ya
ziara yake ya siku tatu nchini humo, kwa kutembelea uwekezaji mkubwa wa
mwekezaji ambaye ameanza ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Mtwara ambacho
kitakuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote
katika Tanzania, kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani za kimetriki milioni
tatu kwa mwaka.
Rais
Kikwete ambaye amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kiwanda hicho na
Bwana Dangote mwenyewe, ameanza ziara yake kwa kutembelea machimbo ya
kiwanda hicho ambayo yako kilomita tisa kutoka kiwandani ambako
malighafi ya kiwanda hicho husafirishwa kwa madaraja na mikada maalum
hadi kiwandani.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kwa sasa Kiwanda cha Obajana
kinazalisha tani za kimetriki milioni 10.25 kwa sasa kwa mwaka na hivyo
kukifanya kiwanda hicho kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani
kilichoko katika eneo moja na kuwa baada ya upanuzi unaoendelea kufanywa
kwenye kiwanda hicho, uwezo wake wa uzalishaji utaongezeka na kufikia
tani za kimetriki 13.0 kwa mwaka ifikapo mwakani 2015.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilicho kwenye eneo
la kilomita za mraba saba kitakuwa kimegharimu kiasi cha dola za
Marekani bilioni 2.5 wakati upanuzi wake utakapokamilika. Kwa sasa
kiwanda hicho kina biashara ya dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kiwanda hicho kilichoanza kujengwa
mwaka 2003 na kukamilishwa mwaka 2006 na hatimaye kuzinduliwa na Rais
Olusegun Obasanjo Mei 12, mwaka 2007, wiki mbili kabla ya kustaafu Urais
wa Nigeria, kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja na hivyo kuwa miongoni
mwa waajiri wakubwa zaidi katika Nigeria.
“Mheshimiwa
Rais, ili kuelewa vizuri mchango wa kiuchumi na kijamii za kiwanda hiki
na viwanda vyetu vingine katika maeneo mengine ya Nigeria, unahitaji
kukumbuka kuwa kabla ya kuanza kujenga kiwanda hiki, Nigeria nzima
ilikuwa na uwezo za kuwazalisha tani za kimetriki za saruji milioni1.5
tu, wakati huo chini ya miaka 10 iliyopita. Tunataka kufikia hatua ya
kuhakikisha kuwa eneo la Afrika Magharibi na hata Bara letu la Afrika
linaacha kabisa kuagiza saruji nje ya Bara letu. Na tutafikia huko.”
Mbali
na Kiwanda cha Obajana, Kampuni ya Saruji ya Dangote inazalisha saruji
katika maeneo mengine mawili ya Nigeria ambalo uzalishaji wa jumla wa
maeneo hayo matatu ni tani za metriki 20.25 kwa mwaka.
Amesema
Bwana Dangote kuwa ili kuweza kuwa na uhakika wa umeme, uongozi wa
kiwanda hicho uliamua kuzalisha umeme wake kwa ajili ya kiwanda hicho
kwa kujenga, miongoni mwa hatua nyingine, bomba ya kilomita 92 la
kusafirisha gesi kutoka Ajaokuta hadi kwenye kiwanda hicho.
Alipoulizwa
na Rais Kikwete kama wanategemea kwa namna yoyote umeme wa taifa, Bwana
Dangote alijibu kwa furaha, “hatujaunganishwa kwenye gridi ya taifa na
tunadhani hili ni jambo zuri kwa sababu hatua tulizochukua
zinatuhakikishia umeme wakati wote na kwa kiwango ambacho tunakihitaji.
Tunatumia gesi ama diseli yetu wenyewe. Na wala siyo umeme tu, hata
miundombinu ya eneo hilo kiliwemo daraja hili kubwa linalonganisha eneo
la machimbi na kiwanda, tumejenga sisi Mheshimiwa Rais.”
Bwana
Dangote amesema kuwa mbali na kujenga miundombinu ya umeme wake,
kiwanda hicho pia kimejenga bwawa lake lenyewe kwa ajili ya huduma ya
maji kusaidia uzalishaji wa saruji bila kutegemea huduma ya maji ya
Serikali. Aidha, bwawa hilo linatoa huduma ya maji kwa jamii
inayozunguka kiwanda hicho.
Mbali
na shughuli za kiwanda, Kampuni ya Bwana Dangote inashiriki kwa karibu
sana shughuli za jamii inayozunguka kiwanda ambacho kwa sasa imeanzishwa
miji midogo saba katika eneo lililokuwa pori lenye nyumba 50 za wenyeji
tu kabla ya shughuli za kiwanda hicho kuanzishwa.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inatoa shughuli za
elimu, maji na umeme kwa wananchi ambao wanazunguka kiwanda ambacho
tokea kuanzishwa kwake limevutia mabenki 13 ambayo yameanzishwa matawi
yake katika eneo la kiwanda. “Mheshimiwa Rais, mbali na nyumba za
wafanyakazi, tunawajengea hata nyumba za kuishi wananchi wanaozunguka
eneo hili ambao wanatuunga mkono sana.”
Mbali
na kutoa huduma nyingine za kijamii, Kampuni ya Saruji ya Dangote
inajenga taasisi kubwa ya elimu ya Dangote Academy ambayo itatoa elimu
na mafunzo ya kiufundi kwa ajili ya kuandaa wafanyakazi wa kiwanda hicho
na watoto wa jamii inayozunguka kiwanda hicho.
Ili
kuhakikisha kuwa upanuzi wa kiwanda hicho unakwenda kwa kasi kubwa
zaidi, Bwana Dangote ameagiza kiasi cha malori 6,000 kutoka China
kusaidia ujenzi na pia amechukua uamuzi usiokuwa wa kawaida wa kuagiza
maelfu ya vibarua kutoka nchi hiyo hiyo ya China kushiriki katika ujenzi
huo na kuumaliza kwa haraka.
Bwana
Dangote amemwambia Rais Kikwete kuwa kampuni yake inafanya jitihada
kubwa kuhakikisha kuwa Rais Kikwete anakifungua kiwanda cha saruji cha
Mtwara kabla ya kustaafu mwishoni mwa mwaka ujao.
Mbali
na Nigeria na Tanzania, Bwana Dangote ana viwanda ama anajenga viwanda
vya saruji ama na shughuli za saruji katika nchi 14 za Afrika ikiwamo
Ethiopia, Zambia, Mozambique, Kenya, Senegal na Sierra Leone, Afrika
Kusini, Congo (Brazzaville), Cameroun, Ghana, Liberia na Ivory Coast.
Mbali
na shughuli za uzalishaji wa saruji, Bwana Dangote ambaye anakubaliwa
kuwa tajiri mkubwa zaidi katika Afrika kwa thamani ya dola za Marekani
bilioni 25 yeye na kampuni yake ya Dangote Group pia ina shughuli za
uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa chumvi, utengenezaji wa magunia,
uzalishaji maji, uzalishaji wa vyakula vya aina mbali mbali, uzalishaji
wa mafuta ya kupikia, utengenezaji wa nyanya. Kwa sasa anaendelea na
ujenzi wa kiwanda cha mbolea na kile cha kuzalisha bidhaa za petrol na
kemikali.
Kampuni
ya Saruji ya Dangote – Dangote Cement- ndiyo kampuni kubwa kuliko zote
katika Afrika Magharibi kwa sasa ikiwa na thamani ya dola za Marekani
bilioni 22.7 kwa tathmini ya mwaka huu baada ya kuongeza thamani yake
kutoka dola za Matrekani bilioni14.5 za mwaka jana.
Mwishoni
mwa ziara hiyo yenye mafanikio makubwa, Rais Kikwete ameondoka Obajana
kurejea nyumbani kupitia Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na
Luanda, Angola ambako kesho (jumamosi) anatarajia kukutana na marais wa
nchi hiyo kabla ya kurejea nyumbani.
No comments:
Post a Comment