Ofisa
Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia) akimkabidhi
moja ya kompyuta Mkuu wa Shule ya Sekondari Azania, Mwl. Benald Ngonzie
(kushoto), wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni wanafunzi wa shule hiyo.
Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye
thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Ofisa
Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia) akimkabidhi
moja ya kompyuta kwa wanafunzi waliowawakilisha wenzao, anayeshuhudia
makabidhiano hayo ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Benald Ngonzie. Benki hiyo
jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi
ya Sh2 milioni.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia)
akimkabidhi moja ya kompyuta makamu wa rais wa shule ya sekondari ya
Azania, Johnson Kaaya, wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa shule
hiyo, Mwl. Benald Ngonzie. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10
kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Azania, Mwl. Benald Ngonzie akiongea na
wanafunzi mara baada ya makabidhiano ya kompyuta kwa shule hiyo
iliyotolewa na Access Bank. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta
10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Ofisa
Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko akiongea na vyombo vya
habari mara baada ya kukabidhi kompyuta kwa shule hiyo. Picha zote na
Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Shule
ya sekondari ya Azania inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ikiwamo
majengo na ubovu wa vyoo, hali inayohatarisha afya za wanafunzi hao
kutokana na kuwapo kwa majimaji anayoweza kuzalisha mbu waenezao ugonjwa
wa Malaria na Dengue.
Akizungumza
jana baada ya kupokea msaada wa kompyuta 10 kutoka katika benki ya
Access, Makamu Mkuu wa shule hiyo Elizabeth Ngoda alisema shule hiyo ni
kongwe kwa sasa kutokana na kujengwa muda mrefu hivyo inahitajika
ukarabati wa kina.
"Shule
ni kongwe na imezalisha viongozi mbalimbali na sasa imechakaa, majengo
yanahitajikukarabatiwa na vyoo havitoshi, lakini tunawashukuru Access
Bank kwa kutuletea kompyuta hizi, kwani tulikuwa na kompyuta 25 awali
ambazo hazikukidhi mahitaji kutokana na kuwa na idadi kubwa ya
wanafunzi," alisema Ngoda na kubainisha kwamba shule ina wanafunzi 2000
na wafanyakazi 115.
Ngoda
alitoa wito kwa wadau wengine pamoja na wanafunzi waliowahi kusoma
katika shule hiyo,kujitolea kwa hali na mali ili kuirudisha Azania
katika hali nzuri ya kimazingira.
Makamu
wa rais wa shule hiyo Johnson Kaaya aliwashukuru wadau hao huku akitoa
wito kwa makampuni mengine kuchangia katika kurekebisha kasoro kadhaa
zilizopo shuleni hapo hasa miundombinu.
"Tunaahidi
kuzitumia kompyuta hizi katika kuleta ufanisi na si vinginevyo,
tunaomba hii iwe chachu kwa makampuni mengine kusaidia zaidi kwani
changamoto kubwa hapa shuleni kwetu ni uchakavu wa majengo, hatuna viti,
vyoo vibovu na pia tunapata taabu kipindi cha joto kwani hakuna feni,"
alisema Kaaya.
Naye
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Muganyizi Bisheko alisema
msaada huo ni katika mwendelezo wa mchakato wa kusaidia sekta ya elimu
nchini hasa katika upane wa teknolojia ya abari na mawasiliano ambayo
imeonekana kuwa kikwazo kikubwa katika utafutaji wa ajira kwa vijana
ambao humaliza shule bila kuwa na utaalamu wa kompyuta.
"Tunaamini
kupitia kompyuta hizi wanafunzi wataweza kujifunza programu mbalimbali
ambazo zitawasaidia katika kukuza elimu yao hapa shuleni na katika
maisha yao," alisema Bisheko.
No comments:
Post a Comment