Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 20, 2014

MAZOEZI YA KARAMA YAMTISHA THOMAS MASHALI




Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese katikati ni katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini PST Antony Rutta picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Karama nyilawila ni bondia anayetegemea kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 may kuzichapa na Said Mbelwa kuwania ubingwa wa UBO (universal boxing organisation) katika ukumbi wa friends corner – manzese. Hapo awali karama alikuwa azipige na Thomas mashali alievunja mkataba wa pambano kwa kutokuwa vema kwa pambano hilo na badala yake nafasi hiyo ikadondokea kwa said mbelwa ambaye ana vigezo vyote vya kugombania ubingwa. Karama Nyilawila akiwa katika mazoezi ya mwishomwisho alisema” Mashali ananiogopa baada ya kusikia mazoezi ninayofanya ni magumu na hatari kwa bondia atakae katiza mbele yangu, kwani kila siku asubuhi lazima nikimbie kutoka sinza ilipo gym yetu mpaka kibaha maili moja kwenda na kurudi na jioni napiga mfuko wa mazoezi(bag) raundi sita za dakika kumikumi na nacheza sparing raundi 15, aliposikia hivyo mdogo wangu mashali ikabidi achomoe kwa kutafuta visingizio mbalimbali na pambano limekuwa likibadirishwa tarehe kwa ajili yake na mwishowe akaweka wazi kuwa ananiogopa.karama aliendelea kwa kusema huyu mbelwa kavamia adhabu ambayo sio yake,asuburi tarehe ifike apate cha kumuhadithia mashali.
Nae kiongozi na mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe amesema siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengi makali ya utangulizi yakiwemo ya  Suleiman tall akizipiga na Abdala pazi, ramadhan kumbele akimvaa morobest, zumba kukwe wakioneshana ubabe  na kamanda wa makamanda, idi athuman na julias kisarawe.
Wakati huohuo ndio tunamalizia makubaliano ya mwisho ya bondia chipukizi na mwanamuziki  mashuhuri wa bendi ya mapacha watatu Halid Chokoraa ambae amekubali kuzipiga na Abdul manyenza katika pambano la raundi nne kilogram 63. chokoraa kwa sasa yupo vizuri sana kwa mchezo wa ngumi na ana uwezo wa kumkabili bondia yoyote wa uzito wake.

SAHEL TRADING CO.LTD wauzaji wa mizani ya aina mbalimbali


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...