Washiriki
wa Miss Tabata 2014 wakiwa kwenye pozi.
Xxxxxxxxxxxxx
Na
Mwandishi Wetu
Shindano
la kumtafuta Redds Miss Tanzania Tabata 2014 limepangwa kufanyika Juni 6 katika
ukumbi wa Da’ West Park.
Mratibu wa
Miss Tabata Joseph Kapinga alisema kuwa warembo 24 watachuana vikali kutaka
kumrithi Dorice Mollel ambaye anashikilia taji hilo.
Dorice pia
ndiye anayeshikilia taji la Redds Miss Ilala.
Kapinga
alisema kuwa warembo hao wanaendelea kujifua katika ukumbi wa Da’ West kila
siku kuanzia saa nane mchana chini ya waalimu wawili, Neema Mchaki na Pasilida
Mandali.
Mratibu
huyo alisema fainali hiyo itasindikizwa na aina mbali mbali ya burudani ikiwemo
wasanii kutoka nje ya nchi.
Warembo
wanaendelea na mazoezi kila siku ni Esther Frank Kiwambo (20), Badra S. Karuta
(20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Nuru Omary Athumani
(19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wenine ni
Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20), Ambasia Lucy Mally (22),
Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna
Ibrahim (19), Ramta Mkadara (20) na Mariam Shwaib Hussein.
Warembo
watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Redds Miss
Ilala baadaye mwaka huu.
No comments:
Post a Comment