Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Young Africans Bw Yusuf Manji
amesema kuondoka kwa wachezaji wao wawili Didier Kavumbagu na Frank Domayo sio
mwisho wa timu ya Yanga, kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya
kuhakikisha inasajli wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye
msimu ujao kwa kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.
Akiongea na waandishi
wa habari makao makuu ya klabu leo, Manji amesema yameongelewa mengi sana kwa
kipindi cha mwezi mmoja ambao hakuwepo nchini kwa ajili ya kazi zake binafsi
lakini sasa amerejea na maandalizi ya msimu ujao yameshaanza.
Kuondoka kwa
Kavumbagu ni kutokana na kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi ya wachezaji
wageni kwa msimu mpya, huku Domayo ambae tangu mwaka jana aliombwa kuongeza
mkataba alikua akisema anamsubiria mjomba wake ndipo aweze kufanya hivyo.
Pamoja na kuondoka
kwa wachezaji hao bado kwa kushirikiana na kocha Hans watahakikisha Yanga
inaendelea kutisha msimu ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa,
Hans aliahidi kuleta wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga siku alipokua
akiiongea na waandishi wa habari kuwaaga.
No comments:
Post a Comment