Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 9, 2014

FIFA yaanika orodha mpya ya viwango duniani


http://www.dailyvedas.com/wp-content/uploads/2014/04/Team.jpgWAKATI Brazil ikipanda kwa nafasi mbili katika orodha ya viwango vya soka duniani hadi kuingia kwenye Top 4, Tanzania yenyewe imeendelea kung'ang'ania katika nafasi ya 122 duniani.
 Brazil wenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu, imezipiku nchi za Colombia na Uruguay waliokuwa wamewatangulia katika mwezi uliopita ikiwa nyuma ya Hispania inayooendelea kuongoza orodha ya FIFA iliyotangazwa leo.
Mbali na Hispania, nchi nyingine zilizoitangulia Brazil ni Ujerumani wanaoshika nafasi ya pili kama orodha ya Aprili na Ureno kadhalika wakiwa nafasi ya tatu.
Katika orodha ya 20 Bora, nyuma ya Brazil kuna Colombia, Uruguay, Argentina, Uswiss, Italiaa, Ugiriki, England, Ubelgiji, Chile, Marekani, Uholoanzi, Ufaransa, Ukraine, Russia, Mexico na Croatia iliyofunga ndimba.
Kwa orodha ya Afrika Ivory Coast imeendelea kuongoza orodha ikiwa katika nafasi ya 21 duniani ikifuatiwa na Misri wanaokamata nafasi ya 24, Algeria (25), Ghana (38), Cape Verde (42), Nigeria (44), Tunisia (49), Cameroon (50), Guinea (51) na Mali (59) waliofunga 10 Bora ya Afrika.
Ukanda wa CECAFA kama kawaida Uganda wameendelea kutisha wakishinda nafasi ya 18 Afrika na 86 Duniani, ikifuatiwa na  Ethiopia wanaokamata nafasi ya 101 Duniani na 27 Afrika.
Nyingine zinazozifuata timu hizo ndani ya CECAFA ni Kenya, Sudan, Tanzania, Burundi, Rwanda, Eritrea, Sudan Kusini, Somalia na Djibout inayoburuza mkia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...