Makamu
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wa Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni,Salum Dosi
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
mashindindano ya Safari Pool Taifa kwa Mikoa mitatu ya kimichezo, Kinondon,i
Temeke na Ilala Dar es Salaam jana.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,
Oscar Shelukindo na Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga
Mchezaji
wa Safari Pool Taifa wa Klabu ya East London Mkoa wa kimichezo wa Temeke , Amos
Boniphace akicheza kuashilia uzinduzi mashindano hayo Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wa Mkoa wa Kimichezo
wa Kinondoni,Salum Dosi akimkabidhi t-shirt mwakilishi wa Klabu ya Jaba wa Mkoa
wa kimichezo wa Kinondoni, Mayaula Muhagama wakati wa uzinduzi wa mashindano ya
Safari Pool Taifa kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambao unajumuisha mikoa mitatu ya
kimichezi, Kinondoni ,Ilala na Temeke.
MASHINDANO ya mchezo wa pool yanayojulikana kama 'Safari Lager National Pool Championship 2012' katika mikoa maalum ya kimichezo ya Temeke, Ilala na Kinondoni yanaanza kutimu vumbu leo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, katibu mkuu wa chama cha mchezo huo nchini (TAPA), Amosi Kafwinga alisema kuwa maandalizi yote katika mikoa hiyo tayari yamekamilika.
Kafwinga alisema kuwa klabu 10 kutoka Temeke, 12 Kinondoni na 12 Ilala zitachuana vikali katika mashindano hayo ngazi ya mikoa ambayo yanadhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager.
Alisema kuwa bingwa wa kila mkoa licha ya kuzawadiwa fedha taslim Sh.700,000 lakini pia atakata tiketi ya kushiriki fainali za taifa za mashindano hayo zitakazofanyika Septemba mkoani Mwanza.
Naye meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema kuwa wao kama wadhamini tayari wamekamilisha kila kitu kinachohusiana na mashindano hayo ikiwa ni pamoja T-shirt na pesa za maandalizi kwa timu zote.
Shelukindo alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha mchezo huo unaenea nchi nzima hasa ikizingatia mwaka jana yalishirikisha mikoa 14 lakini mwaka huu yanashirikisha mikoa 16.
Makamu mwenyekiti wa Baraza la Michezo Wilaya ya Kinondoni, Salim Dossi ambaye ndiye aliyekabidhi T-shirt pamoja na pesa za maandalizi kwa timu zote, aliwapongeza wadhamini wa mashindano hayo bia ya Safari Lager kwa kuweza kuinua mchezo huo nchini.
Dossi aliwataka wadhamini hao kutouacha mchezo huo bali waendelee na juhudi zao za kuudhamini ili nao uweze kuwa moja ya michezo tishio kama ilivyo soka kutokana na kwamba tayari dalili zimeanza kuonekana.
No comments:
Post a Comment