Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 13, 2012

VISHOKA WA WIZI WA UMEME WABAMBWA TEMEKE



Mtuhumiwa wa wizi wa umeme Siwamini Muhammed, akiwa chini ya Ulinzi wa jeshi la polisi na wakaguzi wa Shirika la umeme Tanesco  baada ya nyumba yake ilioko Mbagala kizuiani kukutwa ikiwa imeunganishwa umeme kwa njia ya wizi kabla haujafika kwenye mita nakuutumia bila kuulipia.
(NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Mmoja wa wakaguzi wa mifumo ya umeme Oktavian Mmunyi, akiangalia nyaya zilizounganishwa chini kwa chini kwaajili ya kuba umeme wa Tanesco wakati wa zoezi la ukamataji wezi wa umeme linaloendelea kwenye kanda ya Tanesco Temeke, watu saba wanashikiliwa na eshi la polisi kwa wizi wa umeme.
Sehemu iliyounganishwa umeme kabla haujafika kwenye mita na kusomwa kwenye moja ya nyumba zilizokutwa eneo la Kizuiani Mbagala jijini Dar es Salaa wakati wa Operesheni maalum ya kukamata wezi wa umeme linaloendelea kwenye kanda ya Tanesco Temeke ambapo watu saba wameshikiliwa na jeshi la polisi kwa wizi huo.




WATU saba wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa umeme baada ya kuwakamata kwenye operesheni ya kukamata watu wanaoiba umeme inayoendelea kwenye kanda maalum ya Tanesco Temeke.
Kwenye zoezi hilo ambalo linafanywa na timu maalum ya Tanesco na kusaidiana na Jeshi la Polisi kumegundulika wizi wa aina mbalimbaliikiwemo wakujiunganishia umeme kwa kupitisha waya chini ya aridhi na kujiunganishia kabla haujafika kwenye mita na kusomwa.
Zoezi hilo ambalo leo ilikuwa ni zamu ya eneo la Mbagala Kizuiani liliwapa wakati mgumu wakaguzi wa mifumo ya umeme wa shirika hilo baada ya kufika mtaa wa CCM eneo hilo la kiuzuiani na kukuta nyumba zaidi ya 6 wakitumia umeme kutoka kwenye nyumba moja huku wakiwa wamejiunganishia kwa kuchumbia nyaya chini ya aridhi na wakaguzi hao kuamua kukata kabisa waya zake na kuwashikilia watuhumiwa wa wizi huo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Meneja wakanda hiyo ya Temeke Richard Malaamia, amesema tatizo la wizi nikubwa kwahiyo wanalazimika kufanya zoezi hilo kuwa endelevu hadi wananchi watakapojenga mazoea kutumia umeme kwa kufuata utaratibu.
Malamia amesema wisi wa umeme uekua ukisababisha hasara ya Tsh 89Millioni kwa mwezi na kulikosesha mapato shirika hilo.
Hata hivyo wakaguzi wa mifumo ya umeme walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa wao binafsi walidhani tatizo la wizi wa umeme lipo zaidi kwa watumiaji wakubwa lakini kkutokana na matukio wanayoshuhudia inawapa wasiwasi kuwa kuna idadi kubwa zaidi ya watu wanao iba umeme hata kwa watumiaji wadogo kabisa.
Mkaguzi Daniel Maswi alisema, tabia ya kujiunganishia umeme kabla ya kufika kwenye mita ni hatari na inaweza kusababisha hatari hata ya kulipua nyumba kwani nyaya zinazo tumika ni hafifu mno na umeme unaopita ni mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...