Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa kufuata Sheria za Kiislamu
wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akionyesha kadi ya ATM ya
akaunti ya kiislamu ya benki hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ambayo
wateja wawili wa akaunti hiyo watajishindi tiketi mbili kila mmoja
zitakawawezesha kusafiri kwenda kuhiji Makka mwezi Oktoba. Uzinduzi
huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Baraza Kuu la Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa
Kundecha na kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(BAKWATA) Suleiman Lolila.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha (kushoto) akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kampuni ambayo wateja wawili wa akaunti ya kiislamu ya NBC
watajishindia tiketi mbili kila mmoja zitakazowawezesha kusafiri
kwenda kuhiji Makka kwa gharama za NBC Mwezi Oktoba. Uzinduzi
ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya
Huduma za Kibenki kwa kufuata Sheria za Kiislamu wa Benki ya NBC,
Yassir Masoud na kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) Suleiman Lolila.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo
imezindua kampeni ya miezi miwili kwa ajili ya wateja wake wa huduma za
kibenki zinazofuata sheria za kiislamu, ili kubaini washindi
watakaoshinda Safari ya wawili iliyolipiwa kila kitu kwenda kuhiji Makka
mwezi Oktoba 2012.
Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa katika
Ofisi za Makao Makuu ya NBC ni sehemu ya sherehe za miaka 45 za benki ya
NBC kutoa huduma za kibenki. Sherehe hizi zitawezesha wateja kushinda
zawadi mbalimbali zilizotayarishwa kwa ajili yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu
wa Idara ya kutoa huduma za kibenki kwa kufuata Sheria za Kiislamu wa
NBC, Yassir Masoud alisema,"Kampeni hii siyo tu kwa ajili ya
kusherehekea miaka 45 ya kutoa huduma bora za benki kwa wateja wetu
lakini pia kusherehekea miaka miwili ya kutoa Huduma za kibenki zenye
kufuata sheria za Kiislamu".
"Hii ni mara ya kwanza kwa kampeni ya
aina hii kufanyika nchini na tunawakaribisha wateja wetu wote na yeyote
mwenye nia ya kushiriki, washiriki kikamilifu ili kupata nafasi ya
kushinda zawadi hii ya kipekee" alisema Bwana Masoud.
NBC ilianza kutoa huduma za benki
zinazofuata Sheria za Kiislamu tangu mwezi Mei 2010. Hivi sasa huduma
inayotolewa ni pamoja na Akaunti za Akiba za Kiislamu na Akaunti za
Hundi. Hivi karibuni pia benki ilizindua ya Akaunti za Biashara za
Kiislamu na akaunti za Kiislamu kwa Mashirika. Huduma hizo zinatolewa
bila riba, na kwa kufuata Sheria za Kiislamu, pia ni wazi kwa wateja
wote bila kujali imani zao.
Kampeni iliyozinduliwa leo itaisha
Septemba 13, 2012, ambapo washindi watachaguliwa kwa njia ya droo.
Washindi watajishindia safari iliyolipiwa kila kitu kwa ajili ya watu
wawili kwenda Kuhiji. Zawadi ni pamoja na tiketi za ndege, malazi na
fedha za matumizi wakati wa safari hiyo ya kwenda Makkah.
No comments:
Post a Comment