Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 20, 2012

NGOMA AFRICA BAND YATUMA SALAM ZA RAMBI RAMBI KWA WALIOFIKWA NA MSIBA KATIKA AJALI YA MELI YA SKAGIT



Bendi ya Muziki "Ngoma Africa band" yenye makao yake nchini Ujerumani, Inatoa pole na rambi rambi kwa ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla waliopatwa na msiba kutokana na ajali ya meli ya MV Skagit, iliyotokea jana 18-7-2012 jirani na Kisiwa cha Chumbe, Zanzibar.

Ngoma Africa Band inaungana na watanzania wote walio nyumbani na nje ya nchi katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa kitaifa, msiba huu ni wetu sote. 

Bendi hiyo imamua kutangaza rasmi kusimamisha maonyesho na matamasha yake ilkiwa ni sehemu ya kuomboleza msiba huo kwa muda wa wiki moja.

Mungu ibaraki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...