Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 11, 2012

NMB YAENDESHA DROO YA KWANZA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB


 
Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akifafanua jambo wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mineja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Sadiki Elimsu.
 
 Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akifafanua jambo wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mineja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia
 
Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akibonyeza kitufe kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, sadiki Elimsu na Meneja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia.

DAR ES SALAAM, Tanzania
Baada ya ubinafsishaji wa benki ya NMB mwaka 2005, NMB iliendelea kukuza mtandao wake wamatawi, ndani ya miaka mitano matawi yameongezeka kutoka 100 hadi matawi zaidi ya 140. Idadi ya watejawa NMB imekua kutoka wateja 600,000 mpaka wateja1,600,000 hiyo ni asilimia 30 au 40 ya watanzania wote ambao wana akaunti katika benki zote za Tanzania ili kurahisisha na kuboresha utoaji huduma. NMB ilianza kutoa huduma ya  ATM kutoka wateja 0 mpaka wateja milioni moja na laki sita na pia namba za mashine za kutolea fedha (ATM) zimekuwa kutoka 0 mpaka 450 na pia NMB ndio benki ya kwanza Tanzania kuanzisha huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi, NMB Mobile. Hadi sasa kuna wateja 600,000 wanaotumia huduma ya NMB Mobile
NMB imeendelea kubuni na kuanzisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wateja wake. NMB ndio benki pekee Tanzania yenye akaunti kuanzia za watoto wadogo, wanafunzi, wafanyakazi, wakulima na wastaafu. Pia NMB imeendelea kuboresha faida wateja wanazozipata kutokana na kuwa na akaunti NMB. Hivi sasa mteja wa NMB ana chaguo pana la njia za kupata huduma anaweza kupata huduma ndani ya benki, kutumia ATM, kutumia NMB mobile au huduma ya Intaneti.
NMB ni benki inayowajali sana wateja wake hata wakati washida, mwaka jana, 2011 NMB ilizindua huduma ya NMB Faraja inayomwezesha mteja wa NMB Personal Account kupata mkono wa pole kati ya shilingi 600,000 hadi 1,200,000. Hadi sasa, huduma ya NMB Faraja imewanufaisha wateja wengi wa NMB, nchi nzima.
JENGA MAISHA YAKO NA NMB
Utafiti uliofanywa na NMB uligundua kuwa wateja wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea. Miongoni mwa malengo hayo ni kujenga nyumba, kusomesha watoto na kufikia malengo mengi na muhimu maishani mwao. NMB ikiwa ni benki yenye kujali malengo ya wateja wake, inaanzisha promosheni inayowezesha wateja wote wa NMB Bonus Account na NMB Junior Account kuingia kwenye droo ya kushindania tani ya saruji, mabati ya kuwezekea, amana maradufu, ada za shule, fulana za NMB au mabegi ya shule kupitia promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB. Promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB itachezeshwa kila mwisho wa mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu.
NMB inaamini promosheni hii sio tu kwamba itaongeza tabia ya kujiwekea akiba lakini pia itasaidia wateja watakaoshinda kufikia malengo waliyojiwekea na pia kuboresha maisha yao. Wateja wote watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye NMB Bonus Account au NMB Junior Account watapata riba ya kuvutia ambayo inaweza kuwa hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana zilizowekwa.
Zawadi zinazoshindaniwa kwenye droo ya leo
Zawadi
Namba ya washindi
Tani ya saruji (simenti)
8
Mabati
3
Double your account
3
Mabegi ya shule
100
Ada zashule
3
Tishetiza NMB
150



Kuhusu NMB Bonus Account na NMB Junior Account
NMB Bonus Account niakauntimahususi ya amanakwaajili ya kufikiamalengombalimbali. NMB Bonus Account inaribakubwaunayopatakilarobomwaka.Akauntihiiinakuwezeshakutunzaamanakwausalamanabilagharama
Faidaza NMB Bonus Account
·         Hakunagharama ya kuendeshaakauntihii
·         Huduma ya NMB Bonus Account inapatikanakwamatawizaidi ya 140 nchinzima
·         Unapataribakilarobomwaka, piariba ya ziada*
·         Hakunagharamazakuhamishafedhakutoka NMB Personal Account kwenda NMB Bonus Account au kutoka NMB Bonus Account kwendaNMB Personal Account

NMB Junior Account niakuntiinayofunguliwanamzazi/mlezikwaniaba ya mtoto. Lengo la akauntihiinikumsaidiamzazi/mlezikuwekaakibakwaajili ya matumizi ya baadaye ya kumjengeamtotomsingiwakuwekaakiba

Faidaza NMB Junior Account
·         Kiwangokizuri cha ribapamojanariba ya ziada
·         Hainagharama ya uendeshaji
·         Kumjengeamtototabia ya kuwekaakiba
·         Mtotoakifikishamiaka 18 akauntihiyoitaitwa NMB Bonus Account naataiendeshamwenyewekwafaida
·         Mzazianaruhusiwakutoafedhamarambilikwamwakabilakupotezariba ya ziada
*Mashariti ya uendeshajikuzingatiwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...