Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 8, 2012

SIMBA YAICHAPA YANGA 3-0 WABUNGE



 Mbunge, mshambuliaji wa Yanga, akiwatoka mabeki wa Simba, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Wabunge mashabiki wa Yanga na Wabunge mashabiki wa Simba, uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Wabunge hao walitoka sare ya bila kufungana katika dakika 90 za mchezo na mwamuzi wa mchezo huo Othman Kazi, akaamuru timu hizo kupigiana penati, ambapo Simba wameweza kuibuka kidedea kwa penati 3 kwa 2.
 Mhe. Majaliwa, akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa 'Yanga'.
 Mshambuliaji wa Yanga, akiwatoka mabeki wa Simba.
 Kocha mpya wa Yanga, akiwa katika Benchi la wachezaji wabunge wa Yanga, wakati wa mchezo huo, pamoja na waheshimiwa wabunge wa Benchi la ufundi.
 Wachezaji wabunge wa akiba wa Yanga katika benchi lao.
 Wachezaji wa akiba wabunge wa Simba wakiwa katika benchi lao.
 Wachezaji wa akiba wa Simba.
 Makamisaa wa mchezo huo, Eric Shigongo (kushoto) na Saleh Ally.
 Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
 Mchezo ulikuwa ni Fair Play, hapa mchezaji wa Simba akimhudumia mchezaji wa Yanga, mbele ya mwamuzi Othman Kazi.
 Mara wachezaji walianza kuanguka kwa kukamatwa na misuri, hapa ni Nahodha wa Simba, Amos Makala, akisaidiwa na beki wake, William Ngeleja.
 Kipa wa Simba, Joshua Nassari, akijaribu kuifuata penati bila mafanikio.
 Mchezaji wa Simba, akishangilia baada ya kupiga penati ya mwisho iliyowahakikishia ushindi.
 'Raha ya Ushindi kicheko', Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, akicheka cheko la furaha baada ya kibuka washindi katika mtanange huo.
Shabiki wa Yanga, msanii Dokii, akiwa hoi na nguma yake iliyomshinda uzito baada ya timu yake kuchapwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...