Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 11, 2012

ALLY RHEMTULLAH KUZINDUA MITINDO YAKE MIPYA SEPTEMBA 8 , 2012



Na Andrew Chale
MWANAMITINDO  maarufu nchini, Ally Rehmtullah pichani juu atazindua onyesho rasmi la kazi zake mpya  za mitindo ya mavazi mbalimbali kwa wanawake na wanaume ‘Ally Rehmtullah 2013 Collection’lililopangwa kufanyika Hoteli ya Serena,  jijini Dar es Salaam, Septemba 8 2012.
  Rehmtullah alisema dhumuni la kuandaa onyesho hilo la kipekee ni kuweza kuonyesha aina mpya ya mitindo ya mavazi aliyobuni hivi karibuni na harakati za kuinua kiwango cha kazi za mitindo kwa Tanzania.
“Nimepania kupanua wigo wa taaluma ya mitindo na mavazi hapa nchini,  ili kazi za wanamtindo na wabunifu ziweze kupenya kwenye soko la ndani na la Afrika Mashariki na ya kati wakati tayari kuna soko la pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki,’ alisema.
Pia aliongeza kuwa, kwenye uzinduzi huo mavazi na onyesho litapambwa kwa rangi nyeupe, ubunifu wa hali ya juu pamoja na muonekano mpya wa mavazi yaliyofanyiwa utafiti mkubwa ili kuweza kuendana na utamaduni wa mwafrika.
Aidha, Rehmtullah alisema licha ya kuonesha mavazi pia kutakua na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nyota, ambapo pia aliwataja wadhamini wakuu wa onyesho hilo kuwa, Mercedez Benz, Mo Blog, Belvedere Vodka, Dulux, Raha, Hugo Domingo,The Tanzanite Experience, Shiva Images, Farm Plant, Creative Infinities, Out Door, Stanbic Bank, Phoenicia Properties, Dar es Salaam Serena Hotel, Missie Popular Blog, Quality Furniture na Mx Carter.
Katika onesho hilo, linatarajia kudhuriwa na watu 400, wakiwemo viongozi wa serikali, wafanyabiashara na wageni mbalimbali  ambapo watashuhudia wanamitindo wengine mahili na chipukizi watakaoonesha mitindo siku hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...