Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 1, 2012

Assah Mwambene Mkurugenzi Mpya wa Idara ya Habari - MAELEZO


Bw. Asah Andrew Mwambene ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuanzia tarehe 01 Julai, 2012. Bw. Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Clement Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Bw. Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha, Bw. Mwambene amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo huko Zanzibar.

Idara ya Habari (MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa Serikali hapa nchini.


IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI
NA MICHEZO

AGOSTI 1, 2012

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...