Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 8, 2012

BARAZA LA MADIWANI MUSOMA LAGAWANYIKA, WENGINE WATOKA NJE NA KUSUSIA KIKAO




BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Musoma limegawanyika kwa mara ya kwanza na kufanya baadhi ya madiwani kutoka nje na kususia  kikao baada ya kutofatiana kimtazamo juu ya ugawaji wa halmashauri ndani ya wilaya ya Butiama.
Tofauti hiyo ilitokea jana wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo ambayo makao makuu yake bado yapo ndani ya Manispaa ya Musoma.
Baadhi ya madiwani hasa upande wa  kambi ya upinzani walikuwa wakidai kuwa wananchi wa kata ambazo zimegawanywa na kuwa halmashauri ya Musoma hawatatendewa haki endapo  watakuwa chini ya Mkuu wa wilaya ya Butiama.
Akichangia hoja hiyo diwani wa kata ya Bukima Ruti Mayamba  alisema wawo kama wawakilishi wa wananchi hawatakuwa wamewatendea haki kutoka kata za majita na Lukuba kwani watakuwa mbali na huduma za kiutawala .
Mayamba alisema huduma zitakuwa karibu endapo watakuwa chini ya mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Musoma.
“Tunataka kata hizi kumi na saba ziungane na kata 13 za Manispaa ya Muasoma ili kutengeneza wilaya ya Musoma”,alisema Mayamba.
Kwa upande wa  madiwani  wa chama Tawala waliazimia kuwepo na halmashauri mbili ya Musoma na Butiama ndani ya wilaya ya Butiama ambazo zitakuwa chini ya Mkuu wa wilaya hiyo ya Butiama.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...