Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 7, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MABANDA YA MAONYESHO YA NANE NANE DODOMA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo jinsi ya uzalishaji wa zao la Zabibu kutoka kwa Ofisa Mtafiti Msaidizi wa Kilimo wa Kanda ya Kati Dodoma, Richard Malle, (wa pili kulia) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012. Wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal, Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakiangalia Mhogo aina ya Mumba wenye umri wa miaka (3) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Wa pili (kulia) ni Mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mbegu ya mizabibu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso (kushoto) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal,(wa pili kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi mashine za kukamulia miwa zinavyofanya kazi, kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi ya uandaaji hadi kukamilika kwa Sukari tayari kwa matumizi,kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Wa tatu kutoka (kushoto) ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal.
.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya matrekta ya kuvunia mazao aina ya Mahindi, Ngano na Mtama, wakati Makamu alipotembelea katika maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012.Kulia ni mke wa Makamu Mama Zakhia bilal.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...