Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 15, 2012

UJENZI WA BARABARA ZA MABASI YAENDAYO KASI KUPUNGUZA FOLENI ZA JIJI LA DAR?


Mafundi wa ujenzi wa Barabara wakiendelea na kazi ya uchimbaji eneo la katikati ya barabara za jijini Dar es Salaam, ili kujenga Njia ya Mabasi yaendayo kasi, Hapa ikiwa ni eneo la Mkwajuni Kionondoni, ambapo mawazo ya walio wengi ni kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa njia hizo na kuanza kazi kwa mabasi yaendato kasi basi huenda foleni zikawa ndiyo kikomo kama si kupungua. Je nini mawazo yako Mdau juu ya hili mradi hu utakapokamilika Foleni zitapungua ama zitaongezeka?
 Eneo la Bonde la Mkwajuni Kinondoni, ambalo tayari eneo hili la katikati ya barabara lilikuwa limeachwa 'jembamba' sasa wataalam wanatarajia kutushangaza kwa lipi katika eneo hili, ili kupitisha njia hii ya mabasi yaendayo kasi?
 Hapa ni eneo la Bonde la Kawe, Barabara ya Bagamoyo, mafundi wakiendelea na zoezi la kupachika daraja katika eneo hili la barabara hiyo mpya, je kukamilika kwa barabara hii, kutasaidia kupunguza foleni ama kutaongeza foleni kwa kufanya hata wale wenye majumba yao ya kifahari ambao walijenga na kuamua kuhamia mjini na kuyaacha majumba yao na kupangisha ili kukwepa foleni na wao pia wote si watareja na hivyo kuongeza tena msongamano?
 Hapa ni eneo la Lugalo, ukitokea Mwenge, mafundi wakiwa katika harakati za kujenga daraja jipya na kubomoa lile la zamani.
 Hapa ni eneo la Kimara Barabara ya Morogoro, mafundi wakiendelea na zoezi la ujenzi wa Njia ya Mabasi yaendayo kasi.
  Hii ni sehemu tu ya foleni za asubuhi ya jijini Dar es Salaam, hapa ni Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, eneo la Oysterbay Polisi kabla ya taa za kuongozea magari za Namanga, leo asubuhi.
Je ipo siku Jiji hili la Dar es Salaam, litakuja kuwa kama hivi barabara nyeupeeeee, baada ya kukamilika mradi huo ama itakuwa ni ndoto?? zaidi tembelea  http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...