Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 15, 2012

Ushirikiano na TAMIDA ni muhumu; Serikali


Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Eliakimu Maswi akiwa na Kaimu kamishna mkuu wa wizara hiyo Ally Samaje na mwenyekiti wa Tamida hapa nchini Sam Mollel wakiwa kwenye mkutano wa kujadiliana juu ya Bei elekezi na ushirikiano jijini Arusha 
*****
Mahmoud Ahmad Arusha
Wizara ya nishati na Madini imesema kuwa haina tofauti na TAMIDA kwani chama hicho kinatakiwa kutoa ushirkiano ili kuweza kuipeleka mbele sekta ya madini kukuza na kuinua uchumi kupitia sekta hiyo.

Akizungumza na wafanyabiashara wadogo wadogo wa vito jijini Arusha Katibu mkuu wa wizara hiyo Eliakim Maswi alisema kuwa sekta hiyo ni muhimili wataifa hivyo bei elekezi isiwe ndiyo ya kukwepa  kuilipa mapato serekali na kuwataka wanachama wa TAMIDA kushirikiana na serekali kuwafichua wezi warasilimali zetu.

“Mtanzania mzalendo ni Yule anayeilipa serekali kodi halali nanyi mnafanya hivyo hivyo kuweni macho na wale wote wanaotaka kupandia mgongoni mwenu na mtupe ushirikiano kuwafichua wale wote wanaohujumu sekta hii ya madini”alisema Maswi.

Tamida na wizara wamefikia makubaliano ya kutumia Bei elekezi hapa nchini ili kutatua tatizo la bei linalowakumba wafanyabiashara wadogo hapa nchini na kukuta wanauza bei ndogo kwa wajanja bila ya kuwa na taarifa ya bei iliyoko sokoni kwa wakati huo.

Maswi alisema kuwa zaidi ya usd.2.2 bilioni serkali ilikuwa inaidai kamuni ya TANZANITE ONE kutokana na kodi ya tozo ya mrahaba waliyokuwa wamekwepa kuilipa serekali tokea mwaka 2004

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...