Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 2, 2012

WASHINDI SABA WAKABIDHIWA ZAWADI ZA SBL


Meneja wa bia ya Serengeti bw Allan Chonjo (kushoto) akimpongeza mshindi wa pikipiki zilizokuwa zikishindaniwa katika promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti  Bi Rahma  Rashid Ally aliye juu ya pikipiki yake baada ya kukabidhiwa na meneja huyo. Wengine ni wafanyakazi na wawakilishi wa kampunin ya bia ya Serengeti.


Meneja wa bia ya Serengeti bw Allan Chonjo kulia akimpongeza bw.Joseph Felix aliye juu ya pikipiki yake baada ya kukabidhiwa na meneja huyo. Wengine ni wafanya kazi wa kampuni ya bia Serengeti . Picha namba 8 ni meneja huyo akiwa na wafanya kazi wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na washindi 7 waliokabidhiwa zawadi zao jana jijini Dar.



Kampuni ya bia ya Serengeti jana ilikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni hiyo ijulikanayo kama ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL’ ambapo jana ilifikia tamati kwa kuchezesha droo ya mwisho na kuwapata washindi wa gari moja , bajaj, moja na pikipiki na genereta .
Zawadi zilizokabidhiwa jana jioni ni pamoja na pikipiki mbili na jenereta tano zilizokabidhiwa kwa washindi wa jijini hapa na meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo .
Awali akikabidhi zawadi hizo, meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo  amesema promosheni hiyo imefika tamati na kwamba watanzania wajipange upya kwani kuisha kwa promosheni hiyo ni mwanzo wa maandalizi ya promosheni zingine. “ leo tumefunga rasmi promosheni yetu ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ lakini bado tuna baadhi ya washindi ambao bado hawajapewa zawadi zao kutokana na taratibu za usajili lakini siku chache zijazo nao watakabidhiwa zawadio, sambamba na hilo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa niaba ya kampuni ya bia ya Serengeti kwa wateja wetu juu ya ushirikiano mkubwa waliouonesha kwetu katika kipindi chote cha promosheni yetu” alisema Chonjo.
Kwaupande wao washindi waliokabidhiwa zawadi zao, waliipongeza sana kampuni ya bia ya Serengeti kwa kujitolea kwake kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii na kuisadia kwa njia mbalimbali kama ambavyo imetumia mamilioni ya shilingi kuendesha promosheni kuwa kuliko yote kutokea hapa nchini. “ mimi naishukuru sana sbl kwani promosheni hii sasa imeweza kunitoa katika hali mbaya ya kimaisha na kubadilisha kabisa maisha yangu” aliseama mmoja wa washindi hao ambaye yeye amejishindia pikipiki mpya kabisa.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni  ya “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’, nchi nzima kwa muda  wa miezi minne na Promosheni hiyo imeweza kuleta mabadiliko yakinifu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Serengeti Breweries Limited ni kampuni tanzu ya EABL/ DIAGEO.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...