Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 6, 2012

YANGA YALITEKA BUNGE DODOMA


 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga wa pili kulia akiwa na kocha Mkuu wa timu hiyo, Tom Saintfiet.
Wachezaji wa Yanga wakiwa Bungeni mjini Dodoma.

Na Danson Kaijage, Dodoma

MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, ‘Kagame Cup’ Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo wamepokewa kwa shangwe na wabunge wanazi wa timu hiyo, lakini wakikumbana na kebehi za watani zao, Simba kwa kuwaonesha alama ya vidole vitano walipofanya ziara ya kulitambulisha kombe hilo bungeni.

Licha ya kupokewa kwa kishindo, baadhi ya wale wa Simba nao waliibuka na kuwakebehi kwa kuonesha vidole vitano juu, wakimaanisha kipigo cha 5-0, ilichopokea katika mechi ya kufunga msimu wa Ligi Kuu Bara, msimu uliopita.

Hali hiyo ilitokea wakati Spika, Anne Makinda alipokuwa akitambulisha wageni waliohudhuria bungeni kwa ajili ya kuangalia shughuli zinazoendelea.
Baadhi ya wabunge walionekana kuonesha mikono yao ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.

Wengine ni Mbunge wa Tabora mjini, Aden Rage, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Viti Maalum, Diana Chilolo.

Akitangaza ujio huo wa Yanga, Makinda alisema: “Mimi siku zote huwa natangaza watu ambao wanaleta vitu vizuri bungeni. Hawa Yanga ni wageni mashuhuri kutokana na kuleta vitu vizuri.

“Lakini, mimi nikisema hivi, baadhi ya wabunge wanasema mimi ni mpenzi wa Yanga, kitu ambacho si kweli…Yanga wameleta ubingwa, ndiyo maana nimewatangaza,” alisema Spika Makinda.

Wakati Makinda akitoa kauli hiyo,  baadhi ya wabunge waliangua kicheko, ambapo pia aliongeza: “Namuona Mh. Spika aliyepita (Samwel Sitta), ananiangalia lakini huo ndiyo ukweli.”

Kikosi hicho cha Yanga, kiliambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya klabu hiyo, Fatuma Karume, Francis Kifukwe.

Kwa upande wa uongozi, ni Mwenyekiti Yusuph Manji na Makamu wake Clement Sanga walioingia madarakani Julai 15, kupitia uchaguzi mdogo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...