Kikundi
cha ngoma cha Basesilia Bujora, kikionyesha umahiri wake ambapo
waliibuka washindi wa siku ya mwisho ya tamasha la Bujora ambapo
walishinda na kuibuka na kitita cha shilingi laki mbili na thelathini
baada ya mpinzani wao upande wa pili kutoka Musoma kuingia mitini,
Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia
yake ya Serengeti Premium Lager.Kiongozi wa kikundi cha Basesilia Bujora, akionyesha umahiri wake wa kucheza na nyoka
katika siku ya mwisho wa tamasha hilo ambapo kikundi chake kiliibuka
washindi wa siku hiyo, Tamasha hilo lililodumu kwa takribani wiki nzima
lilivutia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza lilidhaminiwa na kampuni
ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Mkuu wa wilaya ya Magu Ndugu Jacquiline Liana akizungumza na wananchi katika tamasha hilo. Umati
wa wakazi wa Wilaya ya Magu wakifuatilia kwa makini ngoma za jadi
kutoka kabila la wasukuma ‘Bulabo’ katika kiwanja cha Kisesa. Tamasha
hilo lililodumu kwa takribani wiki nzima lilivutia maelfu ya wakazi wa
jiji la Mwanza lilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia
yake ya Serengeti Premium Lager.
Wapiga ngoma za asili wakipiga ngoma Kwa
shangwe kubwa maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Magu jijini Mwanza wamekuwa
wakishuhudia burudani ya ngoma za asili za kabila la wasukuma ’Bulabo’
ambalo limemalizika siku ya Jumapili jioni katika uwanja wa Kisesa
jijini Mwanza. Katika sherehe hizo za kiutamaduni vikundi ishirini na
nane kutoka makabila ya wasukuma vilishiriki na kuzifanya sherehe hizo
zivutie zaidi. Kampuni ya bia ya Serengeti imeahidi kuendelea kudhamini
tamasha la ngoma za kabila la wasukuma ’Bulabo’ ambazo ni maalum kwa
ajili ya kusheherekea sikukuu za mavuno kila mwaka.
“Tunayofuraha
kubwa kwa mara nyingine tena kuona tumeweza kuungana na wenzetu wa
kabila la wasukuma katika kipindi cha wiki moja sasa na kusherehekea
furaha yao baada ya mavuno huku wakiendelea kuzienzi tamaduni zao. Ni
kwa mara ya nane sasa tumekuwa tukidhamini sherehe hizi za bulabo na
tunaahidi kuendelea kudhamini kwani sherehe hizi zina mchango mkubwa kwa
wasukuma na taifa kwa ujumla”. Alisema jaji Mark Bomani mwenyekiti wa
kampuni ya bia ya serengeti.
Kampuni
ya bia ya Serengeti imekuwa ikidhamini tamasha hilo kwa takribani mwaka
wa nane sasa,ambapo waandaaji wameishukuru kampuni hiyo kwa kuwezesha
na kufanikisha tamasha hilo, ”Napenda kutoa shukrani zetu kwa kampuni
ya bia ya Serengeti ambayo imekuwa mdhamini wetu kwa muda mrefu sasa
inafika miaka minane, tumekuwa nao bega kwa bega na hasa Mwenyekiti wa
Bodi ya Kampuni hiyo Mheshimiwa Mark Bomani ambae pia ni mlezi wetu hapa
Bujora” alisema Padri Mhoja, muandaaji wa tamasha hilo.
Naye
mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Jacquieline Liana,
ameipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kudhamini tamasha hilo na
kuomba wadau wengine kujitokeza kudhamini kama wenzao wa kampuni ya bia
ya Serengeti wanavyofanya, pia aliwaasa vijana kuacha tabia za kunywa
pombe wakati wa kazi na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili waje
kusheherekea sherehe hizi za Bulabo mwakani.
Katika sherehe hizo za Bulabo
vikundi vilivyoshiriki vilishindana kwa mtindo wa mtoano ambapo vikundi
viwili vikiwa katika pande mbili tofauti za uwanja vikitenganishwa na
bendera nyekundu, huku majaji wakiangalia ni kundi lipi lenye umati
mkubwa hivyo ni kuashiria kuwa mwenye watu wengi zaidi ndiye mwenye
mvuto zaidi na hapo kutangazwa mshindi. Kigezo kingine kichokuwa
kikiwafanya washiriki waongeze jitihada katika kucheza na kujikuta
wakiwapa raha zaidi watazamaji ni kile cha kundi linaloshindwa kutakiwa
kutoa elfu thelathini katika laki mbili ambazo zilikuwa zikitolewa kwa
kila kundi na kumpa mshindi.
Washindi
katika ngoma hizo zilizodumu kwa takribani wiki moja ni Nghomi Lukala,
Kanigini Hindiya, Kibola Shitungulu, Bagehu Lukala, Mayokagose, Kinasa
Ncheye, Nyamuitabungagwa Mnkoti, Mabeshi Lukwaja, Nyeyewaza, Shigulu
Dema, Bulolo Shokolo, Seleleko na Basesilia Bujora aliyemalizia siku ya
Jumapili baada ya mpinzani wake kuingia mitini.
No comments:
Post a Comment