Mmwanamuziki wa kundi la muziki wa Hip Hop la G-White Juma Abdallah akitumbuiza
mamia ya wapenzi wa muziki wakati wa
tamasha la Coke Zero lililofanyika Jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Mmwanamuziki wa kundi la Hip Hop la G-White Paul Mushi akitumbuiza
mamia ya wapenzi wa muziki wakati wa
tamasha la Coke Zero lililofanyika Jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Wakazi wa Jiji la Arusha na vitongoji vyake walijitokeza kwa
wingi katika viwanja wa Soweto Jumamosi Juni Mosi kushuhudia miondoko ya
wasanii wa muziki wakiongozwa na mkali wa Hip Hop nchini Joe makini pamoja na
kikundi cha G-White.
Tamasha hili lilikuwa maalum kwa ajili wa uzinduzi wa
kinywaji kipya cha Coca-cola Zero kanda ya kaskazini iliyo chini ya kampuni ya
kutengeneza na kusambaza vinywaji baridi jamii ya Coca-Cola ya Bonite Bottlers
yenye makao yake mjini Moshi.
Burudani hiyo ya aina yake ilianza saa nane kwa vijana
waendesha piki piki wakionyesha umahiri wao wa kutawala chombo hicho cha moto kabla
ya kikundu cha Hip Hop kcha Paul Mushi na Juma Adballah kupanda jukwaani na kupokelewa
kwa shangwe na maelfu ya wapenzi wa muziki waliojitokeza kushuhudia tamasha
hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika tukio hilo,
Mkurungenzi Mkuu wa Mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Bw. Christopher Loiruk
alisema kampuni yake inayo furaha kwa kuandaa tamasha hilo kuitambulisha Coke
Zero na kuburudika pamoja na wateja wao.
‘Bonite Bottlers tumekuwa mstari wa mbele kudhamini michezo
pamoja na kuendeleza vipaji vya vijana na leo tumeona kikundi kipya kabisa cha
muziki wa Hip Hop kikipata nafasi ya kuonyesha umahiri. Wapenzi wa muziki watakubaliana
name kuwa wakiendelea kupewa fursa na kuwezeshwa wataweza kuwa moja ya wasanii
wanzuri sana hapa nchini.’ Anasema Bw. Loiruk.
Naye Meneja Bidhaa Coca-Cola Tanzania Maurice Njolowa alisema
nia ya kampuni yake ni kuweka kinywaji kipya cha kampuni hiyo cha Coke Zero
karibu na vijana na kwa kuandaa tamasha la bure kama hivi ndio njia nzuri ya
kuwa karibu.
Tamasha
hilo ni muendelezo wa tamasha la Coke Zero lililofanyika Coco Beach jijini Dar
es Salaam wakati kinywaji hicho kisicho na sukari kilipozinduliwa jijini Dar es
Salaam mwezi wa Machi mwaka huu. Tamasha lingine la Coke Zero litafanyika jijini
Mwanza hivi karibuni
No comments:
Post a Comment