Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akifungua mkutano wa
Shirika la Hifadhi za Mbuga za Taifa TANAPA na wahariri wa vyombo vya
habari kuhusu Wajibu wa vyombo vya habari katika kukabiliana na Ujangili
katika hifadhi za taifa unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo
Ofisi za Manispaa ya Iringa, Balozi Kagasheki amewaasa wahariri wa
vyombo vya habari kujadiliana kwa undani suala zima la kukomesha
ujangili na jukumu la wanahabari katika mkakati huo wakishirikiana na
serikali kwa ujumla kupitia taasisi za ulinzi katika mbuga za wanyama,
amewataka wahariri kuwa wabunifu kwa kuandika makala na habari za
kiuchunguzi ili kuibua mbinu hizo chafu na majangili ili kutokomeza
ujangili huo na kupata ufumbuzi kamili wa changamoto hizo za ujangili,
ameongeza kwamba wizara yake iko tayari kupokea maoni mbalimbali kutoka
kwa wahariri na wadau mbalimbali yatakayofanikisha kupata ufumbuzi wa
kutokomeza kabisa ujangili katika mbuga na pia amejiwekea utaratibu wa
kukutana na waandishi wa habari kila mwezi atakutana na vyombo vya
habari ili kuzungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya wizara
hiyo. Wahariri mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakati akifungua mkutano huo. Wahariri
wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa makini katika kusikiliza wakati
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika mkutano huo. Balozi Khamis Kagasheki akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano huo kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akizungumza katika mkutano
huo wakati akimkaribisha Waziri wa Malisiali na Utalii Mh. Balozi Khamis
Kagasheki.
Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiongozana na
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma wakati akiwasili katika
ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo mkoani Iringa ambako mkutano wa
Wahariri wa vyombo vya habari na Shirika la Hifadhi za mbuga za Taifa
TANAPA unafanyika. Mwenyekiti
wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi Mazingira Ndugu James Lembeli
akiingia kwenye ukumbi wa mkutano huku akiwa ameongozana na Mkurugenzi
wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi kushoto. Waziri
wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kulia
akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi
na Mazingira Ndugu James Lembeli na kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
TANAPA Ndugu Allan Kijazi na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine
Ishengoma.
No comments:
Post a Comment