Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, December 10, 2010

Castle Lager imeanza kudhamini matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya soka, England.


KAMPUNI ya bia Tanzania TBL, kupitia bia yake ya Castle Lager, imeanza kudhamini matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya soka, England.

Matangazo hayo yalianza rasmi Novemba 20, mwaka huu na kuhusisha vituo 48 vya Televisheni barani Afrika, vikiwamo vituo vya hapa nchini TBC1 na StarTV.

Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja, alisema Castle Lager, imekuwa ikidhamini soka kwa zaidi ya miaka 30 na kuifanya ithamini umuhimu wa mchezo huo kwa watumiaji wake.

“Kwa kushirikiana na Ligi Kuu England, Castle Lager, itaweza kujitangaza kikamilifu katika bara la Afrika,” alisema.

Aliongeza “ tunafuraha kuwa sehemu ya tukio kubwa la kimichezo duniani na kuiweka Castle Lager, katika daraja la juu ulimwenguni, tunaamini wateja wetu watafurahia jambo hili.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...