Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 7, 2010

SUPER D ACHUKUWA FOMU YA KOZI YA UKOCHA WA MCHEZO WA NGUMI


Na Victor Mkumbo, jijini

KOCHA wa Ngumi wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila ´Super D´ amechukua fomu kwa ajili ya kushiriki katika kozi ya makocha wa mchezo huo inayotarajiwa kuanza Disemba 14 hadi Disemba 24 mwaka huu.

Akizumza na gazeti hili, Super D amesema kuwa ameamua kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki katika kozi hiyo ambayo itahusisha makocha mbalimbali wa mchezo huo.

Amesema kuwa kozi hiyo itamsaidia kuongeza elimu juu ya mchezo wa ngumi na kuweza kuifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji vya vijana mbalimbali.

´´Nimeamua kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki katika kozi ya makocha ambayo itafanyika mwezi huu ambapo ninatarajia kuwa itanisaidia kuongeza ujuzi ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji kwa vijana ambapo katika kozi hii nimedhaminiwa na Zulfiqar Ali.´´ alisema Super D.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania BFT, Makore Mashaga amesema kuwa fomu za kushiriki katika mafunzo hayo zimeshaanza kutolewa ambapo mpaka sasa wameshachukua fomu makocha watano.

Amesema kuwa fomu za kushiriki katika mashindano hayo zinapatikana kwa sh. 20,000 katika ofisi za BFT na pia ametoa wito kwa wadau na wapenzi wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi.

´´Tumeshaanza kutoa fomu ambapo mpaka sasa wameshachukua fomu watu watano na tunatoa wito wa wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi ili tuweze kufikia malengo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...