Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, December 5, 2010

MBUNGE WA VITI MAALUMU ATOA BURUDAN


Mbunge wa Viti Maalum wa mkoa wa Singida,ambaye pia ni msanii wa nyimbo za Injili, Martha Mlata, ‘Triple M’ amekamilisha wimbo wake maalum wa kumpongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete, kwa ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu uliopita hivi karibuni.

Wimbo huo unaokwenda kwa jina la Hongera Jk, Big Up Jk, umerekodiwa katika Studio za Omega Production 2010, zilizopo Kinondoni Moroco, chini ya mwandaaji ‘Producer’ Amri Hing.

Akizungumza na gazeti hili Mlata, alisema kuwa katika wimbo huo amemshirikisha pia mpiga gitaa mahiri, Alex Sinkamba, ambaye amepiga magitaa yote katika wimbo huo.

Martha alisema kuwa ameamua kutunga wimbo huo wa kumpongeza Rais baada ya kazi kubwa aliyoifanya ya kutangaza Ilani ya Chama cha mapinduzi na kunadi Sera za Chama hicho nchi nzima na hatimaye kuibuka na ushindi wa kuweza kutapa nafasi ya kuwaongoza watanzania kwa kipindi cha pili.

Aidha Martha alisema kuwa wimbo huo maalum, anatarajia kumkabidhi Rais ikiwa ni moja ya zawadi pekee aliyoiandaa kutokana na kuamini kuwa ndiye rais pekee aliyeweza kukubalika na wananchi hadi kufikia kumchagua tena kwa mara ya pili.

“Tunaamini kuwa ushindi wake ulikuwa ni wa haki kutoka kwa Mungu, kutokana na uongozi bora wa awamu ya kwanza ya uongozi wake, na kile kilichopangwa na mungu mwanadamu hawezi kukipangua hivyo kwa ushindi huu wa kutuongoza tena wananchi wa Tanzania, ndiyo maana nimefarijika na kuamua kumtungia wimbo wa kumpongeza.

Kwani Rais Jakaya alishapangwa na mungu kutuongoza, nasema tena hongera Jk, asiyetaka na ahame” alisema Mlata.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...