
Na Josephat Lukaza 
Msanii
 wa Muziki wa Dansi anayejulikana kama Christian Bella anayetamba na 
kibao chake cha Nani Kama Mama ni Mmoja wa Wasanii watakaotoa Burudani 
ya Kufa mtu katika Ukumbi wa Mlimani City Siku ya Jumamosi Tarehe 30 
katika Fainali kubwa ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT).
Bella 
Amehaidi kutoa Burudani ya uhakika ambapo wapenzi wa muziki wake 
watafurahi na kufurahishwa na show atakayoitoa siku hiyo katika Fainali 
ya Kumkabidhi Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kitita
 cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Katika
 Fainali hiyo inayotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Siku
 ya Jumamosi tarehe 30 huku viingilio vya Kuja kutazama fainali ya 
Kwanza kubwa vikiwa ni V.I.P Shilingi 50,000 na Kawaida 30,000 huku 
fainali hiyo ikirushwa live kupitia Kituo cha Runinga cha ITV na milango
 itakuwa wazi kuanzia Saa 7.30 Usiku.
Tanzania
 Movie Talents (TMT) ni shindano la Kwanza kufanyika Afrika Mashariki na
 Kati ambalo limeanzishwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd likiwa na 
lengo la Kuibua na Kusaka Vipaji vya kuigiza kwa watanzania ambao wana 
vipaji lakini walikosa fursa ya kuonekana. TMT ilianza Rasmi tarehe 1 
April 2014 katika Mkoa wa Mwanza, Kanda ya Ziwa ambapo baadae shindano 
likaendelea katika Kanda nyingine Tano huku katika Kila Kanda Washindi 
walikuwa ni watatu huku kanda ya Pwani washindi walikuwa Ni 5 ambapo 
jumla ya Washindi 20 walipatikana na kuletwa Dar Es Salaam katika kambi 
na Hatimaye Mchujo kuanza na Kubakiwa na Washiriki 10 ambao leo hii 
wameingia Fainali ya kuzisaka zile Milioni 50 za Kitanzania.
Katika
 Fainali hiyo Kubwa kutakuwa na Burudani kutoka kwa wasanii 
mbalimbali.Sikiliza Moja ya Nyimbo atakazoimba Live Stejini Siku Hiyo ya
 Fainali
No comments:
Post a Comment