Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 3, 2014

HAWA NDIYO WASANII WAKALI ZAIDI BONGO


Kutoka kushoto, Irene Paul, Jacklyne Wolper na Riyama Ally
WAKATI Elizabeth Michael 'Lulu' akitajwa kama msanii wa kike wa filamu anayependwa na watu kupitia tuzo za 'Tanzania People's Choice Award', Jacklyne Wolper na Irene Paul wametajwa ndiyo wakali zaidi kati ya wasanii wa kike nchini.
Lulu alishinda tuzo mwezi uliopita sambamba na King Majuto na watangazaji wengine wa redio na runinga.
Hata hivyo katika utafiti uliofanywa na MICHARAZO kwa mwezi mmoja kwa kuhoji mashabiki wa filamu wasanii Wolper, Irene, Riyama Ally, Irene Uwoya, Shamsa Ford na Bi Hindu ndiyo  'walifunika' miongoni mwa waigizaji wa kike nchini.
Irene Paul, Shamsa na Wolper ndiyo waliotajwa mara nyingi na mashabiki wakifuatiwa na Riyama, Irene Uwoya, Bi Hindu, Mariam Ismail, Cathy, Sandra na Aunty Ezekiel.
Irene Paul ametajwa kama mmoja wa wasanii wa kike wenye kipaji halisi na wanaojua kugeukageuka katika nafasi yoyote na kusifiwa kupitia filamu za Fiona na 'Kibajaj'.
Uwoya yeye alipata kifyagio kupitia 'Ngumi ya Maria' na Apple wakati Wolper alifunika kupitia 'Ulimi' na 'Ndoa Yangu' aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba.
Kwa upande wa waigizaji wa kiume waliotajwa kufunika ni  Jacob Stephen 'JB', Mohammed Mwikongi 'Frank', Kulwa Kikumba 'Dude', Nurdin Mohammed 'Chekibudi' na Amri Athuman 'King Majuto'.
Wengine katika 10 Bora ni Salum Mboto, Jimmy Master, Mtunisi, Gabo wa Zagamba na Mzee Jengua.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...